ads

Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Thursday, January 15, 2015

WIVU WA MAPENZI WAZUA BALAA MKOANI SHINYANGA

Mkazi  wa mtaa wa Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga Regina  Shija (55) ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga kichwani  na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi.
Afisa mtendaji wa Mataa huo, Bw. Rafael Jumanne ameiambia paparazi kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 5.00 usiku ambao watu wasiofahamika walivamia nyumbani kwa  Regina akiwa  anajiandaa kulala na wajukuu wake wawili.
Amesema baada ya watu hao ambao idadi yao haijafahamika, kuvamia nyumbani hapo walianza kumkatakata mapanga mama huyo kichwani na  mkono wa kulia hali iliyosababisha kuvuja damu kwa wingi baadaye kufariki dunia.
Afisa Mtendaji huyo amedai kuwa chanzo cha  mauji hayo bado hakijafahamika ingawa yanahusishwa na wivu  wa kimapenzi na kwamba   jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu huyo na kuupeleka kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Justus Kamugisha  amethibitisha kutokea kwa tukio  hilo ambapo amesema hakuana mtu yeyote anayeshikiliwa na kuwa jeshi hilo linaendelea na upelelezi huku akiwaomba wananchi kulisaidia kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kulisaidia kuwabaini wahusika na hatimaye kuwakamata na kuwafikisha  katika vyombo vya sheria.

Sunday, June 1, 2014

Download New Video Ayzo Dey ft PNC Shino - Nipe Utamu


Sunday, February 16, 2014

LIL KIM ATARAJIA KUITWA MAMA SIKU ZIJAZO KUTOKANA NA HALI ALIYOKUWA NAYO KWAKIPINDI HIKI

Lil Kim karibuni atakuwa
mama
Rapper kutoka Marekani
amewashangaza karibu kila
mmoja mara baada ya
kuwasili kwenye Blonds Fall
2014 fashion presentation siku
ya Jumatano 12 February
2014, akionyesha accessory
yake mpya "Mimba"
Lil Kim, 39 ,aliwasili katika
event hiyo akiwa na nguo
ndefu ya velvet nyeusi, koti la
manyoya la pink na buti za
Hello Kitty .

Baadae Lil Kim ali-perform
kwenye after party na kutangaza
ujauzito wake

“I’m a mom, but I can turn it
up a little! I’m still going to
work. I’m still going to be
hardcore, the baby has made
me even more of a beast!” she
said while rubbing her bump.