ads

Thursday, May 8, 2014

JUA SABABU 10 ZINAZO SABABISHA MAPENZI KUPUNGUA

Habari zenu wadau wa blog hii,naamini umzima na unafurahia darasa hili la watu wazima,Hebu leo tuangazie mambo 10 yanayo sababisha mapenzi kupungua

Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.


Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-

1.       UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.

2.       USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.


Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.

3.       ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi. 

Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo,  Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.

4.       DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.

Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri  au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja Suala La Ndoa/Kuishi Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa Mwanamke Kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.

Sunday, April 27, 2014

COMING SOON MC SAIBA KUTOKA KISIBASHARESKY SASA AJA NA SONG IKO POA

Msanii wa miondoko ya hip hop kutoka kisibasharesky katika usimamizi wa yuskiss kisiba ambaye kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya kutoa nyimbo yake inayokwenda kwa jina la IKO POA
Msanii huyo (MC SAIBA) Amesema ``kwa sasa najiandaa kutoa nyimbo hii pia na nyingine itafuata hivi karibu ambayo tunategemea video yake kufanyia nchini ghana kwa usimamizi wa yuskiss kisiba ambaye ndiye anaye jaribu kutimiza ndoto za watu wengi hasa kwa wasanii kwani ni producer na anaweza mambo mengi sana``Baada ya hapo yuskiss kisiba naye alisema kuwa ameamua kufanya kazi na Mc saiba kwani nikijana anaye jituma pia anakipaji na uandishi mzuri wa mashairi.Pia kisiba aliongezea kwakusema kuwa ana muandaa producer ambaye naye yupo katika lebo yake kwajina anajulikana kama DOBE GUY.
Pia anapenda kuwa karibisha vijana kwaajili yakutimiza ndoto zao popote pale walipo kwani Kisibasharesky entertainment haishughuliki na kitu kimoja ila kuna vitu vingi sana ndani yake.
https://www.facebook.com/pages/Yuskiss-Kisiba
https://www.facebook.com/ykisiba

Tuesday, April 22, 2014

KISIBASHARESKY SASA YAJA KATIKA MTAZAMO MPYA WA TUMAINI ZA KUTIMIZA NDOTO ZA WENYE VIPAJI AINA ZOTE SOMA HAPA KUFAHAMU ZAIDI

Yuskiss kisiba Kiongozi wa kampuni inayo jihusishana mambo mbalimbali mtandaoni na kisanaa KISIBASHARESKY ENTERTAINMENT ambaye CSW tulifanya mahojiano naye baada ya kuanzisha kitengo utengenezaji wa musiki.Yuskiss alisema ameamua kufanya hivyo kutokanana wasanii wengi wamekuwa wakihitaji msaada kutoka katika tasnia ya film na video lakini wanashindwa kutokana na msaada unakuwa mdogo kwa upande wao pia akaongeza kwa kusema kuwa kwa yoyote mtu mwenye kipaji ambaye atakuwa anajiweza na anajiamini hatosita kufanya nae kazi.
kwa sasa kisibasharesky inahusikana Utengenezaji wa video,graphics,photograph katika majarada na mitindo ya mavazi,Utengenezaji wa midundo aina zote (Beat) Matangazo aina zote mtandaoni,Blog design Pamoja na Cover aina zote Cd,dvd n.k.
kiongozi huyo anawakaribisha sana wale wote watakao penda kushirikiana naye.
kwani mpaka sasa kuna baadhi ya vijana tayari wamesha anza kazi
kama masanii Mc saiba na Dobe guy ambapo hivi karibuni kazi zao zitatoka kuanzia mtandaoni na media pia.

==Imeandikwa na Marry kutoka CSW.==

Friday, April 4, 2014

HAPPY BIRTHDAY DERRICK SWAG

Leo mwenyekiti wa kundi la Cash point jijini mwanza anasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwake.
Kwakuonesha utofauti wa hali ya juu katika sherehe yake ambapo Ameambatana na wanakikundi wenzie chief Yuskiss kisiba,Jay 4 shizo manizo,Issa dody, simple girl pamoja na mashabiki wanao penda kundi hilo lenye mtazamo tofauti wa kimaisha Ambapo kundi
.Kundi hilo limepiga hatua katika masoko afrika mashariki katika swala la ujasiriamali  pia wameweza kumiliki kampuni zao binafsi kama COM,KIDO TZ Vijana hawa wamekuwa wakifanya vitu vya kipekee katika jamii kwa kuwasaidia watu mbalimbali
misaada pia Cash point imekusanya Vipaji mbalimbali kwakila aliyeomo ndani ya kundi kwakuwatembelea wodi ya wazazi kwakutoa misaada mbambali kwa wakina mama walio jifungua siku yaleo.
Huuni mfano wa kuigwa kwa vijana wa kiyanzania ambao wanaopenda kujiinua kiuchumi kwakuhakikisha wana pambana na umaskini hapa nchini bila ya kutegemea ajira serikalini.

==HAPPY BIRTHDAY DERRICK SWAG==

Thursday, April 3, 2014

MASANJA MKANDAMIZAJI AZIDI KUNG‘ARA ZAIDI AIBUKA NA MKOKO MPYAAA TENA WAGHARAMA MSOME HAPA

UTAJIRI wa komediani maarufu nchini  Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.HABARI MEZANIAwali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake.“Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake.MAGARI SITAIlibainika kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa.NYUMBA TATU BONGOPia, mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwaoMbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.MASHAMBA KIBAOMsanii huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lilelililopo Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI ZAIDI?Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwakwenye namba za juu za wasaniiwa maigizo wenye mkwanja mrefu.Wengine wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.MATAJIRI BONGO FLEVAKatika muziki wa Bongo Fleva, wasanii wanaoaminika wana utajiri mkubwa zaidi ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.Wasanii hao wanamiliki mijengo ya maana, achilia mbali magari ya kifahari na miradi kadhaa.MASWALI KUHUSU MASANJAUtajiri wa Masanja umeonekanakuibuka ghafla huku vyanzo vyake vya kumwingizia kipato vikijulikana ni sanaa ya uigizaji, muziki na huduma ya uchungaji.Je, kwa uigizaji tu katika Kundi laOrijino Komedi ‘OK’ ndiko alikopata mkwanja huo na kuanzisha miradi hiyo mikubwa?Kama ndiyo, kwa nini memba wenzake ndani ya kundi hilo hawana maendeleo makubwa kama yeye?Kazi nyingine ya Masanja ni muziki wa Injili ambapo kwa sasa albamu yake ya Hakuna Jipya iko sokoni. Je, albamu hiyo na shoo anazofanya zinaweza kuwa chanzo cha utajiri huo?Lakini pia Masanja ni mchungajiambaye anahudumu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’ lilicho chini ya Askofu Bruno Mwakiborwa. Je, mshahara anaoupata kutokana na huduma hiyo unaweza kuwa chanzo cha mapato yake?Risasi Mchanganyiko halikutaka kupasua kichwa, juzi lilimsaka Masanja kwa simu na kumhoji juu ya mali zake ambapo kwanza alithibitisha kweli anamiliki mali hizo na nyingine ambazo hakupenda kuzitaja.“Ni kweli nina nyumba tatu hapa mjini, kampuni ya ulinzi na mashamba ya mpunga eka 50 nyumbani Mbarali, Mbeya. Kuhusu magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni mtumishi sitakiwi kusema uongo,” alisemaMasanja.

Sunday, March 30, 2014

VIDEO YA “CHUNA BUZI” YA SHILOLE NI MOOOOTOO…!!! ICHEKI HAPA (18+ AGE


Download Maisha ya mjini new Video:Kitifa ft.Linex the voice


Tuesday, March 25, 2014

Mwanafunzi wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Makongo afariki dunia katika ajali mbaya ya Bajaji naLori jijini Dar

Mwanafunzi wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Makongo, PriscusMallya, amefariki dunia katika ajali iliyolihusisha lori na Bajaj katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Bamaga, Dar. Kwa mujibu wa watuwaliokuwa eneo la tukio wakati ajali hiyo ikitokea, wamesema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ndani ya Bajaj pamoja na wenzake wawili wakielekea shuleni Makongo ambapo walikutana uso kwa uso na lori kisha kumrusha na kutokea upande wa pili marehemu.

DIAMOND ATOA YAKE YA MOYONI KUHUSU KUFUNGIWA KWA NYIMBO ZA WASANII WA HAPA BONGO..!! SOMA KAULI ALIYOITOA HAPA

Diamond Platnumz ndiye msanii aliyetajwa sana kuwania tuzo za KTM2014 katika vipengere kama 6 lakini ameamua kufunguka mtazamowake juu ya BASATA kuhusu kufungiwa kwa baadhi ya nyimbo za wasanii , kupitia katika akaunti yake ya instagram Diamond amefunguka na kuandika maneno mengi ya Busara zaidi kuhusu BASATA.Tazama hii picha uone alichofungukaNANUKUU"ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje... Hii ni sawa na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu... Will the target of reaching our goals ever be achieved?? #Ni_Mtazamo_tu"MWISHO WA KUNUKUU

MDADA HUYU AJIUZA KUPITIA FACEBOOK, AKESHA AKIPOST PICHA ZA UTUPU

AnaitwaNEEMA PAUL MALIMOni jina analotumia Facebook, amekuwa ndio Tabia yakekuweka picha za kuwatega wanaume na kuwataka wampigie simu ili aweze kuwapa penzihilo kwa maelewano.Huyu inasemekana ni kahaba wa kutupwa kwani amekuwa akiweka picha zake zisizo na maadili na Ni biashara yake anayoifanya na soko lake anategemea FACEBOOK….!!!!EWE MWANANCHI JIHADHARI UKIMWI UNAUA…

HUYU NDYO MWANAFUNZI ALIYEJIRUSHA KUTOKEA GHOLIFANI MPAKA CHINI UDOM KISA SOMA HAPA

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24, Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo chaSayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na pajila uso.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamshna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote  kujibu shitaka la kujaribu kujiua.Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Sunday, March 23, 2014

Mama ajifungua watoto 11. Bofya"LIKE" kumpongeza Kwani hii ni Rekodi.!

Monday, March 17, 2014

MMMMH!! MWENYE MACHO AAMBIWA TAZAMA EBU NJOO UCHEKI MAMBO YA TABORA LAANA DUNIANI KWA UFUSKA HUUHAPANA DADA ZETU MMEZIDI SASA NI FULL KUONYESHA MAUNGO WAZI.

Hii ni sehemu za baadhi ya picha zilizoonesha nini kilichofanyika katika ukumbi wa Theophilo Kisanji Tabora ikiwa nimoja ya Show zilizoambatana na Shindano lakumsaka Miss & Mr.Kamna .

SERIKALI YA NIGERIA IMEKIRI MAKOSA AMBAYO YALISABABISHWA NA MKANGANYIKO KATIKA ZOEZI LA KUWAAJIRI WATU KAZI KATIKA MIJI NCHINI

Serikali ya Nigeria imekiri makosa ambayo yalisababisha mkanyagano wa watu pale walipokuwa wakihudhuria zoezi la serikali la kuwaajiri watu kazi katika miji kadhaa Nchini Nigeria.Maelfu ya watu waliokuwa na hamu kubwa ya kupata ajira, walijitokeza kwa wingi katika zoezi la mitihani ya kutafuta kazi kote Nchini humo.Walikuwa wamejitokeza katika ofisi za wizara ya uhamiaji.Watu saba waliuawa katika uwanja wa taifa mjini Abuja.Waziri wa mambo ya ndani Abba Moro, aliambia CSW kuwa utaratibu ulikosekana katika uwanja huo kiasi cha kusababisha vurumai hilo.Zaidi ya thuluthi moja ya watu walio chini ya umri wa miaka 25 hawana ajira nchini Nigeria.

Sunday, March 16, 2014

MASKINI MTOTOANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE KISA....

Mtukioyakikatili yameendelea kushika kasi wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mtoto aitwayeSaid Siraji/SaidJoshuaamelazwa katika Hospitali ya wilaya usiku wa kuamkia leo, baada ya kunusurika kifo katika jaribio la kuchinjwa nababayake mzazi aliyejulikana kwa jina laSalvatory.Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya-Kahama; DaktaJosephFwoma amesema Siraji amefikishwa hospitalini hapo leo alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia huko akivuja damu shingoni.Dakta Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.Kwa mujibu wamamamzazi wa Mariamu Idd(35) amesema, Mtoto Siraji jana alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwisha achana siku nyingi.Mariam amesema, awali Salvatory alikuwaakimchukua Sirajimarakwa mara na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye kumrudisha akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya.Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha tukio hilo inasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa akili.

Saturday, March 8, 2014

PICHA ZA DULLY PAMOJA NA MISS MOROGORO ZINAZOLETA UTATA HIZI HAPA.

Thursday, March 6, 2014

Picha 6 za Nicki Minaj zinazoangaliwa sana hivi sasa kwenye mtandao...!

Unaambiwa Nicki Minaj anajipanga kuja na muonekano mpya pamoja akijiandaa na kutoka na album au mixtape.Mara nyingi picha zinazotoka kwenye media zinazomuonyesha Nicki Minaj akiwa na muonekano wa Barbie kama kawaida yake. 

Lakini hizi picha alizozitoa mwenyewe ameonekana kuwa na nywele zake mwenyewe bila vitu vingine anavyojitupiaga.


HATARII..MFUNGWA AMBAKA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI HUKO GEITA...!!!


MFUNGWA aliyekuwa
akitumikia kifungo cha miezi
sita katika Gereza la Butundwe
wilayani Geita amembaka
mwanafunzi wa Shule ya
Msingi Luhuha iliyoko Tarafa
ya Butundwe na kumuumiza
sehemu zake za siri, shingoni
na kwenye jicho la kulia.
Mwanafunzi huyo mwenye
umri wa miaka 15 (jina
linahifadhiwa) alitendewa
unyama huo na mfungwa
aliyejulikana kwa jina la
Godfrey Seleman (19) Februari
26, mwaka huu majira ya saa
9:00 alasiri wakati
mwanafunzi huyo alipokuwa
akichanja kuni na wanafunzi
wenzake.
Akieleza jinsi alivyofanyiwa
unyama huo, mwanafunzi
huyo alisema alipotoka shuleni
akiwa na wasichana wenzake
watano walikwenda kuchanja
kuni ndipo walipomuona
mfungwa huyo akiwa amevaa
sare, lakini baadaye alitoweka
ghafla na kurudi akiwa
amejipaka masizi usoni, akiwa
uchi kisha kuanza kumfukuza
yeye huku wenzake wengine
wakifanikiwa kukimbia huku
wakipiga kelele.
Alisema alizidiwa mbio na
mfungwa huyo ambapo
alimshika kisha kumkaba
shingoni na kumwangusha
chini na kuanza kumtendea
unyama na kumsababishia
maumivu makali sehemu zake
za siri.
“Baada ya kutendewa unyama
huo nilitoka eneo hilo ambapo
njiani nikutana na mama
mmoja nikamwelezea mkasa
ulionipata alinionea huruma
ambapo alinipeleka ofisi ya
kijiji ambako niliandikiwa
barua kuwahi polisi,
nikapelekwa hospitali ambako
walinifanyia vipimo,” alisema
binti huyo.
Aliendelea kusema kuwa
mfungwa huyo alimpiga na
kumuumiza katika jicho lake la
kulia ambalo limevimba na
kuwa bado anasikia maumivu
makali jichoni na
shingoni.Kamanda wa polisi
mkoani hapa amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo
ameliita la kinyama
lisilopaswa kutendwa na mtu
mwenye akili timamu.Alisema
mfungwa huyo mweye na
namba 244/2013 alikuwa atoke
kifungoni mwezi ujao, tayari
ametiwa mbaroni na
atafikishwa mahakamani
upelelezi utakapokamilika