ads

Thursday, January 15, 2015

WIVU WA MAPENZI WAZUA BALAA MKOANI SHINYANGA

Mkazi  wa mtaa wa Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga Regina  Shija (55) ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga kichwani  na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi.
Afisa mtendaji wa Mataa huo, Bw. Rafael Jumanne ameiambia paparazi kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 5.00 usiku ambao watu wasiofahamika walivamia nyumbani kwa  Regina akiwa  anajiandaa kulala na wajukuu wake wawili.
Amesema baada ya watu hao ambao idadi yao haijafahamika, kuvamia nyumbani hapo walianza kumkatakata mapanga mama huyo kichwani na  mkono wa kulia hali iliyosababisha kuvuja damu kwa wingi baadaye kufariki dunia.
Afisa Mtendaji huyo amedai kuwa chanzo cha  mauji hayo bado hakijafahamika ingawa yanahusishwa na wivu  wa kimapenzi na kwamba   jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu huyo na kuupeleka kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Justus Kamugisha  amethibitisha kutokea kwa tukio  hilo ambapo amesema hakuana mtu yeyote anayeshikiliwa na kuwa jeshi hilo linaendelea na upelelezi huku akiwaomba wananchi kulisaidia kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kulisaidia kuwabaini wahusika na hatimaye kuwakamata na kuwafikisha  katika vyombo vya sheria.

Sunday, January 11, 2015

MWANZA!!! Get ready Kwa mara ya Kwanza Kabisa!

MWANZA!!! Get ready for the ‪#‎STEPUP2014‬.... Kwa mara ya Kwanza Kabisa!!!, Hapa @diamondplatnumz MONDI hapa NAPPY BOY! @Tpain you Better save the Date!..21| 02 |2015

Sunday, June 1, 2014

Download New Video Ayzo Dey ft PNC Shino - Nipe Utamu


Saturday, May 31, 2014

KITIFA ft. RICH MAVOKO Unacheza na nani [Audio]

Thursday, May 8, 2014

JUA SABABU 10 ZINAZO SABABISHA MAPENZI KUPUNGUA

Habari zenu wadau wa blog hii,naamini umzima na unafurahia darasa hili la watu wazima,Hebu leo tuangazie mambo 10 yanayo sababisha mapenzi kupungua

Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.


Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-

1.       UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.

2.       USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.


Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.

3.       ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi. 

Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo,  Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.

4.       DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.

Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri  au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja Suala La Ndoa/Kuishi Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa Mwanamke Kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.

Sunday, April 27, 2014

COMING SOON MC SAIBA KUTOKA KISIBASHARESKY SASA AJA NA SONG IKO POA

Msanii wa miondoko ya hip hop kutoka kisibasharesky katika usimamizi wa yuskiss kisiba ambaye kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya kutoa nyimbo yake inayokwenda kwa jina la IKO POA
Msanii huyo (MC SAIBA) Amesema ``kwa sasa najiandaa kutoa nyimbo hii pia na nyingine itafuata hivi karibu ambayo tunategemea video yake kufanyia nchini ghana kwa usimamizi wa yuskiss kisiba ambaye ndiye anaye jaribu kutimiza ndoto za watu wengi hasa kwa wasanii kwani ni producer na anaweza mambo mengi sana``Baada ya hapo yuskiss kisiba naye alisema kuwa ameamua kufanya kazi na Mc saiba kwani nikijana anaye jituma pia anakipaji na uandishi mzuri wa mashairi.Pia kisiba aliongezea kwakusema kuwa ana muandaa producer ambaye naye yupo katika lebo yake kwajina anajulikana kama DOBE GUY.
Pia anapenda kuwa karibisha vijana kwaajili yakutimiza ndoto zao popote pale walipo kwani Kisibasharesky entertainment haishughuliki na kitu kimoja ila kuna vitu vingi sana ndani yake.
https://www.facebook.com/pages/Yuskiss-Kisiba
https://www.facebook.com/ykisiba

Tuesday, April 22, 2014

KISIBASHARESKY SASA YAJA KATIKA MTAZAMO MPYA WA TUMAINI ZA KUTIMIZA NDOTO ZA WENYE VIPAJI AINA ZOTE SOMA HAPA KUFAHAMU ZAIDI

Yuskiss kisiba Kiongozi wa kampuni inayo jihusishana mambo mbalimbali mtandaoni na kisanaa KISIBASHARESKY ENTERTAINMENT ambaye CSW tulifanya mahojiano naye baada ya kuanzisha kitengo utengenezaji wa musiki.Yuskiss alisema ameamua kufanya hivyo kutokanana wasanii wengi wamekuwa wakihitaji msaada kutoka katika tasnia ya film na video lakini wanashindwa kutokana na msaada unakuwa mdogo kwa upande wao pia akaongeza kwa kusema kuwa kwa yoyote mtu mwenye kipaji ambaye atakuwa anajiweza na anajiamini hatosita kufanya nae kazi.
kwa sasa kisibasharesky inahusikana Utengenezaji wa video,graphics,photograph katika majarada na mitindo ya mavazi,Utengenezaji wa midundo aina zote (Beat) Matangazo aina zote mtandaoni,Blog design Pamoja na Cover aina zote Cd,dvd n.k.
kiongozi huyo anawakaribisha sana wale wote watakao penda kushirikiana naye.
kwani mpaka sasa kuna baadhi ya vijana tayari wamesha anza kazi
kama masanii Mc saiba na Dobe guy ambapo hivi karibuni kazi zao zitatoka kuanzia mtandaoni na media pia.

==Imeandikwa na Marry kutoka CSW.==