ads

Saturday, February 1, 2014

VIONGOZI WA DINI, VIJANA VIJANA WAHASISHA UVUMILIVU NA UMOJA KATIKA KAUNTI YA KWALE

Wakati Keya Kazungu alipofanya
ziara ya kurudi katika mji wa
nyumbani kwenye Kaunti ya Kwale
kwa ajili ya mapumziko ya
Krisimasi, aliona mabadiliko ya
kipekee.
Mwezi Januari 2011 wakati
alipoondoka kwenda kusoma Chuo
kikuu cha Nairobi, alisema vijana
wa jirani kutoka dini mbalimbali
yalijichanganya pasipo shida,
wakizungumza wakati wa jioni.
Wakati aliporudi, Kazungu,
mwenye umri wa miaka 25,
alisema aligundua kwamba
marafiki zake walikusanyika kwa
mujibu wa mashirikisho ya dini
zao.
Pasipo kutambua mvutano wa
kidini ulioshamiri, Kazungu,
Mkristu, alisema aliungana na
kikundi cha rafiki zake Waislamu.
"Nilifurahi kuwaona kwani
hatukuwa tumeonana kwa kipindi
cha karibia miaka miwili," Kazungu
aliiambia Sabahi. "Nilitarajia
wangekuwa na furaha pia, hata
hivyo, rafiki zangu walikuwa
tofauti. Kwa dakika kadhaa kikundi
kilitawanyika kwenda eneo
lingine."
Hassan Mwalulu, mwenye umri wa
miaka 24, mkaazi Mwislamu wa
Kwale, alithibitisha kwamba
shughuli za kijamii ziliathiriwa na
mvutano wa kidini katika eneo
hilo.
"Vijana ambao walikuwa wakicheza
pamoja bila kujali dini zao kwa
sasa wanaenenda tofauti,"
aliiambia Sabahi.
"Vilabu vya ndani vya mpira wa
miguu vimeundwa kwenye
mwelekeo wa kidini," alisema,
akiongezea kwamba miezi
michache iliyopita mashindano ya
ndani ya michezo yalikuwa na
maovu ya mtindo wa kidini na wa
kimadhehebu.
"Ni jambo la kawaida kusikia timu
ikisema kwamba 'tutawaonyesha
hawa Wakristo namna mpira wa
miguu unavyochezwa' au
'tutawashinda hawa Waislamu,'"
alisema. "Michezo kama ya mpira
wa miguu inajulikana kwa
kuzidisha mambo mengi ikiwa ni
pamoja na dini, lakini siyo Kwale."
Kubadilisha mwelekeo huo, vikundi
visivyo rasmi na watu binafsi
wanahamasisha shughuli za
mwingiliano baina ya dini katika
kaunti hii, Mwalulu alisema.
"Waliandaa zoezi la kusafisha mji
mara mbili na mashindano ya
[mpira wa miguu] ambapo
wachezaji kutoka imani mbalimbali
wanachanganyika kuunda timu,"
alisema, akiongeza kwamba
jitihada zinaonyesha matunda
taratibu wakati mvutano
unapungua.
Zaidi ya hayo, alisema, vijana
wanakutana katika mikutano
mbalimbali ili kujadili masuala
yanayoiathiri kaunti na jinsi
yanavyoweza kushughulikiwa
vizuri.
"Tumeishi kwa pamoja kwa [muda]
mrefu ili kuruhusu baadhi ya
masuala kutugawanya," alisema.
"Nina marafiki Wakristo ambao
niliwaalika kupata pamoja chai na
vitafunwa nyumbani kwangu au
sehemu ya kulia chakula. na wao
walifanya hivyo hivyo. mvutano
huu wa dini ni suala la kupita.
Tunajitolea kurudisha undugu."
Mauaji ya wahubiri wa dini
yaharibu uhusiano
Hussein Khalid, mkurugenzi
mtendaji wa Haki Africa, asasi
isiyo ya kiserikali ambayo
inatangaza haki za kijamii na
kiuchumi kwa Wakenya wote,
aliiambia Sabahi kwamba mauaji
yasiyo na ufumbuzi ya wahubiri wa
Kiislamu na kikristo yalikuwa
yanaharibu uhusiano.
Khalid alisema serikali inaweza
kupunguza mvutano wa kidini kwa
kuchunguza na kuwashtaki
watuhumiwa wa mauaji ya
mapadri wawili wa Kikatoliki na
wahubiri saba wa Kiislamu katika
mkoa wa Pwani tangu 2012.
Ukosefu wa mashtaka umeongeza
mvutano katika dini mbili, ambazo
matokeo yake wafuasi wake
wamekuwa wakituhumiana wao
kwa wao, Khalid aliiambia Sabahi.
"Tunahisi kwamba vikosi vya ulinzi
vinahusika na mauaji ya watu
wanaotuhumiwa kuwa na
uhusiano na magaidi lakini
wanasababisha matatizo zaidi kwa
jamii ambazo zimekuwa zikiishi
pamoja kwa miaka mingi,"
alisema.
Kamishna wa kaunti ya Kwale
Evans Achoki alikanusha tuhuma
kwamba serikali ilikuwa inahusika
na mauaji nje ya mahakama ya
watuhumiwa wa ugaidi.
"Sote tumeshangazwa na mauaji
lakini uchunguzi unaendelea,"
aliiambia Sabahi. "Hatutoi nafasi
yoyote. Baadhi ya magaidi
wanaweza kuwa wanawalenga
wahubiri katika mpango wa
kuchochea mivutano ya kidini."
Mwenyekiti wa Baraza la Wahubiri
wa Dini mbalimbali wa Pwani
Padri Wilybard Lagho alikiri
kulikuwa na kuongezeka kutengana
na kutovumiliana baina ya imani
tofauti.
Uhusiano kati ya Waislamu na
Wakristo katika mkoa wa Pwani
umetetereka, aliiambia Sabahi.
Msingi wa kuondoa kutokuwa na
uvumilivu wa kidini ni kuendelea
kuonyesha umoja miongoni mwa
viongozi wa dini, alisema,
akiongeza kwamba watumishi
kutoka imani zote wanafanya kila
wawezalo kuboresha uhusiano.
Licha ya kufanya kazi tofauti na
jamii zao, ushirikiano kati ya
Waislamu na Wakristo unahusisha
kuonekana pamoja katika
mikutano inayofanyika katika
ukumbi wa mji na barabarani
kuhubiri amani na umoja , alisema
Lagho.
"Hatuelewi kiwango cha kutokuwa
na uvumilivu, lakini pamoja na
maulamaa wa Kiislamu
tunaonekana kwa utulivu na
uvumilivu pamoja na imani zetu
zinazohusika. Tunaamini kwamba
kutokuwa na uvumilivu wa dini
hakutapunguza vurugu za kisekta,"
alisema Lagho.
Lagho alisema Wakristo
wanahamasishwa kujichanganya
na kufanya biashara pamoja na
Waislamu.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Ushauri la Waislamu Kenya Sheikh
Juma Ngao alisema Maulamaa wa
Kiislamu wataendelea kutetea njia
zisizosababisha vurugu kwa
kutatua mambo.
"Dini zote zinamhitaji kila mmoja
kwa ajili ya ustawi wa dini na nchi
kwa ujumla," aliiambia Sabahi.
"Kuna njia ambazo zinahitaji
kutumika … Bila kujali mtu alikosa
kiasi gani, sio haki kufanya hivyo
kwa mtu wa imani tofauti."
Ngao alisema maimamu kutoka
katika misikiti mbalimbali
wamekubali kusisitiza mada hiyo
ya umoja na uvumilivu wakati wa
mahubiri yao.
"Kuwepo kwa amani ndiyo
kulikuifikisha nchi umbali huu na
tunawajibika kuudumisha,"
alisema.

WAUZA NGUO ZA NDANI MITUMBA WAIZIDI UJANJA TBS JIJINI MBEYA

WAFANYABIASHARA wa nguo
za ndani zilizo hafifu maarufu
kama mitumba jijini Mbeya,
jana waliwazidi ujanja
maofisa wa Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) kwa
kuficha nguo hizo wakati wa
operesheni ya kuzikusanya na
kuwakamata wauzaji.
Wafanyabiashara hao
walioonekana kupewa taarifa
ya nini kitafanyika kabla
walificha nguo hizo hatari kwa
afya za wavaaji na baada ya
kumalizika kwa uparesheni
wakazirejesha sokoni na
kuendelea kuziuza kama
kawaida huku wakijigamba
kuwa Serikali haiwawezi.
Awali maofisa wa TBS
walioambatana na askari wa
Jeshi la Polisi na waandishi
wa habari, waliendesha
operesheni ya kukamata nguo
za ndani hususani chupi,
sidiria na soksi katika masoko
ya Sido na Mwanjelwa lakini
hawakufanikiwa kukamata
hata nguo moja katika
masoko hayo yaliyo maarufu
kwa uuzaji wa nguo za
mitumba ikiwemo zilizokuwa
zikitafutwa.
Ajabu ni kuwa
wafanyabiashara hao
walionesha kuwa na taarifa ya
kufanyika kwa operesheni na
kila kona ya masoko hayo
walisikika wakizungumza kuwa
maofisa wa TBS na polisi
wako katika eneo lao
wakifanya operesheni ya
kukamata nguo hizo.
“Umewaona ndio hao
wamekuja kwa ajili ya
kukamata zile nguo. Lakini
wanatafuta tu ukorofi kama
wanataka kukamata nguo za
mitumba si wakamate tu na
mashati basi.
“Kwa nini watilie mkazo
kwenye nguo za ndani pekee?”
Walisikika wafanyabiashara
katika baadhi ya vibanda vya
masoko hayo mawili wakihoji
hali iliyoonesha kuwa hawana
elimu ya kutosha juu ya
athari za kuvaliwa kwa nguo
hizo.
Mahali pekee walikofanikiwa
maofisa hao ni katika Soko la
Mbalizi ambako walifanikiwa
kumkamata mfanyabiashara
mmoja Lusekelo Adam akiwa
anauza soksi za mtumba na
kumfikisha ofisi ya Kamanda
wa Polisi mkoani Mbeya na
kisha kuteketeza soksi hizo
ambazo muuzaji alisema
zilikuwa na thamani ya Sh
200,000.
Akizungumza mara baada ya
kumalizika kwa operesheni
hiyo Ofisa Viwango na
Mkaguzi wa TBS, Paul
Manyirifa alikiri zoezi hilo
kufanyika kwa
wafanyabiashara walio
wadogo na kusema shirika
linaamini wapo
wafanyabiashara wakubwa
ambao ndio huziingiza kwa
njia za panya na kuwataka
wajisalimishe.
Kwa upande wake
Mwanasheria wa shirika hilo,
Baptista Bitao alisema
adhabu kwa mtu yeyote
anayeuza nguo hizo ni kati ya
Sh milioni 50 hadi 100 lakini
pia Mkurugenzi Mkuu wa
shirika ana mamlaka ya kutoa
adhabu isiyopungua Sh
milioni 20.
Naye Kamanda wa Polisi
mkoani hapa Ahmed Msangi
aliahidi kuendelea kutoa
ushirikiano wa kina kukamata
nguo hizo akisema lengo ni
kuona Watanzania hawawi
watu wa kupokea vitu
vitakavyolisababishia hasara
Taifa lao kwa kuingia
gharama ya kutibu maradhi
yatokanayo na nguo hizo.

Friday, January 31, 2014

KOCHA WA MANCHESTER DAVID MOYES AJIVUNIA KUWA NA NGUVU MPYA UWANJANI BAADA YA USAJILI WA JUAN MATA KULEJEA

KOCHA wa Manchester
United, David Moyes
amesema usajili wa Juan
Mata na kurejea kwa Robin
van Persie na Wayne Rooney
kumerudisha morali Old
Trafford.
Van Persie amerejea uwanjani
baada ya kukosa mechi 11
kutokana na kuwa majeruhi
na kufunga katika ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Cardiff,
huku Mata akifanya kazi nzuri
baada ya kusajiliwa kwenye
dirisha dogo kwa pauni
milioni 37.1 akitokea Chelsea.
"Morali yangu imerudi, kwa
sababu najua kwamba
wachezaji wazuri wamerudi,"
alisema Moyes.
"Lakini bado nataka kushinda
na kucheza vizuri zaidi kwa
hiyo usidhani kwa sababu
nimeshinda leo (juzi) ndio
sababu ya kufurahi".
"Nina furaha kwa pointi tatu
nilizopata lakini wapi, nataka
kwenda na malengo ya wapi
nataka timu yangu icheze,
bado nahisi nina kazi kubwa
ya kufanya".
Ushindi huo umeifanya
Manchester United izidishe
ushindani katika kuwania
nafasi ya nne dhidi ya Everton
na Tottenham, lakini bado
wana tofauti ya pointi sita
dhidi ya timu inayoshika
nafasi ya nne Liverpool baada
ya kikosi hicho cha Brendan
Rodgers kuifunga Everton.
Na Moyes alikiri kwamba ujio
wa Mata, ambaye alicheza
vizuri licha ya kufanyiwa
mabadiliko kunampa namna
ya kupanga timu yake.
Katika mechi dhidi ya Van
Persie alifunga bao la kwanza
kabla Ashley Young hajafunga
bao la pili na la ushindi.
United imepoteza mechi nne
kati ya sita za mwisho
ikifanya vibaya kwenye Ligi na
kwenye makombe mbalimbali.
"Juan alifanya vizuri sana
ametengeneza nafasi nzuri
sana katika dakika 30 za
mwanzo," aliongeza Moyes.
"Tutamtumia na yeye
atatutumia, nilitaka kuwaona
yeye na Robin pamoja usiku
huu (juzi)," alisema.

JOSEPH OWINO ATAMBA KUVAA TIMU YA JKI OLJOLO

MLINZI wa Simba, Joseph
Owino amefurahishwa
kurejeshwa kwenye kikosi cha
timu hiyo na yupo tayari
kuivaa timu ya JKT Oljoro ya
Arusha kesho. Owino
alitofautiana na Kocha Mkuu,
Zdravko Logarusic kwa kile
ambacho kocha alidai kuwa
mchezaji huyo wa kimataifa
wa Uganda, alikuwa hajitumi
katika mazoezi.
Kutokana na hali hiyo,
aliamua kumpeleka Owino
kufanya mazoezi na timu B
kwa maelekezo maalumu.
Owino ambaye kwa sasa
amerejeshwa kundini baada
ya kuomba msamaha,
alisema atafuata maelekezo
ya kocha kama anavyotaka na
kusisitiza kuwa hatoruhusu
kutokuelewana tena kujirudia.
“Mimi ni kama binadamu
wengine na katika hali ya
kawaida watu hutofautiana na
hivyo nafurahi tumemaliza
tofauti zetu na tutafanya kazi
poa,” alisema Owino jana Dar
es Salaam.
Akizungumzia hali hiyo,
Msemaji wa Klabu ya Simba,
Asha Muhaji alisema ni
utaratibu wa kawaida kwa
kocha kuwarejesha wachezaji
kwenye timu B hasa pale
mchezaji anapotofautiana na
kocha.
“Kwa kiasi fulani naweza
kusema kuwa hakukuwa na
lolote baya kubwa ila ni hali
ya kawaida kwa watu
kutofautiana ila kizuri ni
kwamba wameshamaliza
tofauti zao na kwa sasa kila
kitu sawa,” alisema Muhaji.
Kwa upande wake, Kocha
Logarusic alisema anataka
kuona nidhamu ikichukua
mkondo wake katika klabu
hiyo hasa kwa wachezaji
kujituma na kufuata
maelekezo yake.
Katika mchezo huo wa kesho
kati ya Simba na maafande
hao wa Arusha, utakuwa ni
wa pili kwa kocha huyo katika
ligi na kisha timu itakwenda
Morogoro kuivaa Mtibwa
Sugar, Februari 5, mwaka
huu.

TANZANIA YAZIDI KUNG'ARA KIMATAIFA KWAKUWA NA MIRADI MIKUBWA YA KIMAENDELEO

TANZANIA imeendelea kupata
miradi mikubwa ya
maendeleo ya kimataifa,
ambapo sasa imeibuka kuwa
mshindi kimataifa na
kukubaliwa kuanzisha mradi
mkubwa wa Kanda ya Kati wa
Uchukuzi. Mradi huo
utakaohusisha miundombinu
ya reli, barabara na bandari
unatarajiwa kuanza
kutekelezwa wakati wowote
nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana,
Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe,
alisema mradi huo ulishinda
miradi 51 ya nchi zingine za
Afrika katika mkutano wa
Uchumi wa Dunia (WEF)
uliofanyika Januari 22 jijini
Davos, Uswisi.
Kabla ya ushindi huo, mradi
huo uliingia kwenye miradi 16
bora kati ya 51 ya Afrika na
kushindanishwa katika
mkutano huo uliohudhuriwa
na nchi kubwa kiuchumi,
kampuni za kimataifa na
mashirika makubwa ya fedha
duniani.
“Kwa kweli ilikuwa neema na
furaha kubwa kwa Tanzania
kupewa heshima hii, kwani
miradi mingine 16
iliyowasilishwa katika
mkutano huo nayo ilikuwa na
sifa nzuri, lakini mradi huu
wa Kanda ya Kati ambao
takribani asilimia 95 ya
utekelezwaji wake itanufaisha
Tanzania, ulionekana bora
zaidi,” alisema Dk
Mwakyembe.
Kutokana na ushindi huo, Dk
Mwakyembe alimwomba
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
aunde Tume maalumu ya
kitaifa, itakayosimamia na
kushughulikia kikamilifu
utekelezaji wa mradi huo, ili
uwe wa mfano Afrika na
duniani kote.
Sifa zilizochangia mradi huo
kutangazwa mshindi kati ya
miradi bora 16 ya Afrika na
aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Uingereza, Gordon Brown, ni
pamoja na mikakati
iliyowekwa na Serikali ya
Tanzania chini ya Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa
(BRN) ya kuendeleza Ukanda
wa Kati wa Uchukuzi.
Nyingine ni dhamira ya dhati
ya Serikali ya Tanzania
iliyoonekana, pamoja na
mfumo iliyojiwekea katika
utekelezaji wa mradi huo
unaolenga kupanua bandari
za Tanzania na kufungua zaidi
milango ya kiuchumi kwa nchi
jirani.
Alipopewa nafasi ya
kuzungumza baada ya mradi
huo kutangazwa kushinda
katika mkutano huo,
Mwakyembe alishukuru
washiriki wa kila pembe ya
dunia, kwa kuiamini Tanzania
na kuelezea mikakati ya
utekelezaji wa mradi huo
ambapo hata hivyo
alibainisha upungufu wa
fedha uliopo.
Alisema baada ya kuelezea
changamoto zilizopo katika
hotuba yake, Brown
alimtaarifu kuwa mwaka huu
viongozi wakuu wa nchi
duniani, watakutana Abuja,
Nigeria, kupokea tathmini ya
utekelezaji wa mradi huo
ambapo pia itafanyika warsha
ya maandalizi ya utekelezaji
wa mradi mwanzoni mwa
Aprili nchini.
“Tuna mpango wa kumwomba
Rais Jakaya Kikwete awe
mgeni rasmi katika ufunguzi
wa warsha hii, ili
tuuthibitishie ulimwengu
utayari wa Tanzania kuleta
mapinduzi katika sekta ya
uchukuzi,” alisisitiza Dk
Mwakyembe.
Aidha, alisema kupitia warsha
hiyo, Tanzania imejipanga
kuionesha dunia kuwa na
mipango mizuri na ndiyo
maana akaombwa Waziri
Mkuu aunde Tume
itakayofanya kazi kwa saa 24
kusimamia utekelezaji wa
mradi huo.
Alisema alipendekeza tume
hiyo ya watu wanane ihusishe
wataalamu kutoka wizara za
Uchukuzi, Ujenzi, Fedha,
Shirika la Reli Tanzania (TRL)
na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mradi huo kwa Tanzania
utagusa Bandari ya Dar es
Salaam, maeneo ya
Mashariki, Magharibi na
Kaskazini mwa nchi na
utahusisha nchi za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
Rwanda na Burundi.
Miradi mingine Mradi huo
mkubwa ni kielelezo kingine
cha heshima ya Tanzania
kimataifa, ambapo mwaka
jana wakati wa ziara ya Rais
wa Marekani nchini, Barrack
Obama, nchi ilipata heshima
nyingine ya kutekeleza mradi
mkubwa wa umeme
unaojulikana kama ‘Power
Africa’, utakaoinufaisha nchi
na kuwa kitovu cha uzalishaji
wa nishati hiyo.
Katika mradi huo
unaowezeshwa na Marekani
kwa kushirikisha Serikali na
sekta binafsi, una lengo la
kuiwezesha nchi kuongeza
kiwango cha uzalishaji
sambamba na kupata umeme
wa uhakika, utakoongeza
ajira. Serikali ya Marekani
ilitoa dola bilioni 7 kusaidia
kupatikana megawati 10,000
za nishati hiyo, huku sekta
binafsi ikitoa dola bilioni 9.
Moja ya kampuni kubwa
zinazohusika na mpango huo
ni General Electric (GE),
ambayo imekuwa mstari wa
mbele kuhakikisha mradi
unaendelea kwa kuahidi kutoa
megawati 5,000 kwa gharama
za kawaida kwa Tanzania na
Ghana.

Rihanna and Shakira Sizzle in "Can’t Remember to Forget You" Video

Shakira's back and she's belly
dancing on walls again, this time
with Rihanna by her side. The pop
stars unveiled the stunningly
beautiful visuals for their
collaboration, "Can't Remember to
Forget You" and it's got us all
talking.
"It's very reggae and it has a lot
of the vintage feel at the same
time," The Voice coach told VEVO
News about her post-break up
confessional. "That's why I
thought that Rihanna would be the
perfect feature in this song; her
voice in this song is just unreal
because she is reggae. I don't
think I've ever heard a female
singer deliver her lines in a reggae
song with such authenticity, you
know?"
The video, which features the pop
divas lamenting about their
"selective memory" as they dance
their way through a mansion and
its outdoor pool, was directed by
Joseph Kahn, who worked with Rih
Rih and Eminem for "Love the Way
You Lie."
The song is the lead single from
Shakira's self-titled, 10th studio
album, expected Mar. 25 with
more collaborations including Ne-
Yo, "who's out of this world," she
said.
Audio for the "Can't Remember to
Forget You" was released Jan. 13,
and it has so far climbed to No.
28 on the Billboard charts.
Combine the rapidly rising chart
success with the popularity of the
single's Spanish language version
and an Instagram post of her
baby boy that garnered 2.1 million
likes, Shakira has made a return
to Billboard 's Social 50 chart,
which ranks "the most popular
artists on YouTube, Vevo,
Facebook, Twitter, SoundCloud,
Wikipedia, Myspace and
Instagram." It's her first time atop
the chart since this time last
year.
This is her first album since 2010's
Sale el Sol .
"I love proving to myself with
every album that I can still do it,"
Shakira admitted, after saying that
she "always suffers" through the
creative process. But she's
"extremely happy" with how her
album came out. "It's always
nerve-racking, it's always the
same feeling, the same butterflies
in your stomach. You never know
how your body of work is going to
be received ... [but] at the end of
the day, I feel like I have an album
that I wanted to have."

MBOWE NAWENZAKE ASHIKILIWA NA JESH LA POLISI KWAMAHOJIANO MKOANI MBEYA

Chenyekiti wa Chadema Mh.
Freeman Mbowe na wabunge wawili
wa chama hicho Mh. Halima Mdee
na Peter Msigwa wameshikiliwa na
kuhojiwa kwa muda na Jeshi la
polisi mkoani Iringa kwa madai ya
kuzidisha muda katika mkutano
wao wa jana.

PICHA ZA YALIYOJIRI KWENYE MAZISHI YA MZEE DUDE

ALIYEKUWA MUIGIZAJI MCHEKESHAJI KWENYE KIPINDI CHA TV "FUTUHI"KILICHOKUWA KIKIRUSHWA NA STAR TV YA JIJINI MWANZA,MAREHEMU MZEE OMARY MAJUTO@DUDE AMEZIKWA RASMI JANA JIONI JIJINI MWANZA,
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA YALIYOJIRI KWENYE MAZISHI HAYO JANA JIONI,

MAZOEA YA WADADA WENGI WA SASA KUTOKA BILA KUVAA KUFULI YAMUUMBUA MCHEZA TENISI MAARUFU NCHINI MAREKANI NA DUNIANI SERENA WILLIAMS, AZIANIKA NYETI ZAKE MBELE KADAMNASI,

PICHA YA KIHASARA HASARA YA MCHEZA TENISI MAARUFU NCHINI MAREKANI NA DUNIANI KWA UJUMLA SERENA WILLIAMS ZIMEVUJA MTANDAONI,
KWA HARAKA HARAKA IMESHINDWA KUELEWEKA KUWA NI MAKUSUDI AMA NI BAHATI MBAYA KWA YEYE KUONEKANA KUTOKA AKIWA BILA KUFULI,PICHA INAYOMUONYESHA WAZI SEHEMU ZAKE NYETI,
HALI HII IMEKUWA NI KAWAIDA KWA WASANII NA WATU MAARUFU HASA WA JINSIA YA KIKE KUKUTWA NA KAMERA ZA MAPAPARAZI SEHEMU TOFAUTI DUNIANI WAKIWA BILA KUFULI JAMBO LINALOONYESHA KUWA HALI HIYO YA KUTOVAA KUFULI KWA WADADA SASA HIVI NI FASHION.

PICHA,YALIYOJIRI KWENYE MAZISHI YA MPIGA TUMBA MAHIRI NCHINI TANZANIA MASOUD MOHAMED"MCD",

MWANAMUZIKI {MPIGA TUMBA} MAARUFU NCHINI TANZANIA MASOUD MOHAMED "MCD"AMEZIKWA RASMI JANA WILAYANI MOSHI MKOANI KILIMANJARO ALIKOKUTWA NA UMAUTI,MAREHEMU MCD ALIZIKWA JANA MAJIRA YA SAA SABA MCHANA KWENYE MAKABURI YA NJORO,WILAYANI MOSHI MKOANI KILIMANJARO,MAREHEMU  ALIFARIKI DUNIA JUZI JUMATATU MAJIRA YA SAA NNE USIKU KATIKA HOSPITALI YA KCMC{KILIMANJARO},IKIWA NI MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI HAPO KWA MATIBABU BAADA YA HALI YAKE KUWA MBAYA,HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MAZISHI YA MAREHEMU MCD JANA MKOANI KILIMANJARO,