ads

Saturday, February 22, 2014

UTANDAWAZI UMEKUWA NI CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI YA WANAFUNZI BARANI AFRIKA

HABARI za tokea wiki iliyopita. Ni
matumaini yangu kwamba
wanafunzi mnaendelea vizuri na
masomo na wasomaji wengine
wa safu hii Mwenyezi Mungu
anawabariki ili mambo yetu
yaende sawa sawa.Hili ni kama
hitimisho la mada yetu, ile
tuliyojadili kuhusu chanzo hasa
cha watu wazima kujihusisha
kimapenzi na watoto wa shule,
hasa wa sekondari na vyuo.
Kama ilivyotokea wiki iliyopita,
idadi ya wadau waliowasiliana na
mimi ilikuwa kubwa na uchangiaji
wao wa mada ulikuwa ni wa
kupendeza kabisa.
Kama ilivyokuwa awali, bado
lawama zilielekezwa kwa pande
zote mbili, yaani wapo
waliowalaumu vijana wa shule na
wale watu wazima. Mtakumbuka
tulijaribu kuuliza ni kitu gani
kifanyike, ambacho kwa maoni
yenu kinaweza kupunguza tabia
hii, kama siyo kumaliza kabisa.
Ingawa kila mmoja alijitahidi
kushauri vile anavyoweza, lakini
kwa ujumla watu wote walielekea
kuamini kuwa endapo tamaa
ikiepukwa, ya kihali na kimwili,
kati ya wanafunzi na watu
wazima, tatizo hili linaweza
kupungua kwa kiwango kikubwa.
Watoto wa kike wakiondoa tamaa
za maisha mazuri na kupata vitu
vinavyowazidi umri, kama vile
simu za bei mbaya na wazazi nao
wakiamua kudhibiti tamaaa zao
za mwili, upo uwezekano wa
kuondoa tatizo hili.
Utandawazi nao umechangia
sana watu kubadili aina ya
maisha tunayoishi. Tofauti na
zamani, ambapo mtoto mdogo
alikuwa ni mali ya jamii husika,
sasa hivi jukumu la kulea na aina
ya maisha limeachwa kwa mzazi.
Ndiyo maana wakati wapo baadhi
ya watoto wanamiliki simu za bei
mbaya walizonunuliwa na wazazi
wao, wapo wanafunzi ambao
hawatakiwi, siyo tu kumiliki, bali
kukutwa na chombo hicho cha
mawasiliano wakiwa bado shule.
Hata wazazi nao, hawaonekani
kuvutiwa na ule msemo wa
mtoto wa mwenzio ni wako pia,
wanawakuza wa wenzao na
kujisikia fahari kutembea nao.
Mtu mmoja alipendekeza watu
kumrejea Mungu, kwani mambo
haya ya ukisasa, yametufanya
sasa tusione haya kuwa na
wapenzi ambao tumepishana
sana.
Zifuatazo ni baadhi ya sms za
wasomaji wengine na
mapendekezo yao.
“Mimi ni dereva wa chuo kimoja
cha Biblia, karibu yetu kuna
shule moja ya sekondari, siku
moja nilipokuwa natoka tu na
gari niliwaona wanafunzi wawili
wanaokaa nilikokuwa naelekea,
nikasimama na kuwapa msaada,
mmoja akaomba simu ampigie
ndugu yake baada ya kuiona
ndani ya gari, nikampa si
akajibip, nikamuuliza mbona
anajibip akasema mawazo sijui
yalikuwa wapi, baada ya hapo
alianza kunitumia sms
mbalimbali, nilipogundua shida
yake nikamtaka tukutane, unajua
nilimpeleka kanisani na
nikamwambia hapa ndio
nyumbani kwetu, nikamtaka
aokoke, nikamfanyia maombi, je
kama ningekuwa sijaokoka!
Miye kwa maoni yangu tufanye
hivi, ili tuweze kukomesha yule
mtu anapokuwa gesti, yaani
mapokezi inatakiwa awe
anatazama umri wa mzee na
denti mwenyewe, je huyu denti
anaweza kweli kushea love na
huyo mzee? Kama ataona
haiendani hiyo love basi
amwambie yule baba au denti
mwenyewe kuwa hampaswi
kuingia kwenye chumba, akikataa
huenda hiyo itasaidia.
Kama nilivyochangia kuwa hili
jambo ni Comprehensive sana,
udhibiti wake unahitaji nguvu
kubwa mno kwani uhuru mkubwa
tulionao ambao umechangiwa na
Globalization pamoja na social
influence inakuwa si rahisi sana,
ila tunapaswa tu kumrudia
Mungu na kurejea maadili yetu ya
kiasili. Nyorido H A, Kisongo
Arusha.
Anko miye naona wazazi wawe
makini na watoto wao, pia
wanafunzi wajitambue, waache
kujidhalilisha kwa watu wazima.
Mwanafunzi unawezaje
kuchanganya elimu na masomo?
Jamani wanafunzi amkeni kuweni
makini, magonjwa ni mengi sana
na pia wanafunzi anaweza
kuharibu maisha yake endapo
atapata mimba na hao watu
wazima huwa hawakubali hizo
mimba.
Anko hili tatizo kiukweli siyo
rahisi kama unavyodhani,
kilichopo sisi wenyewe tuingiwe
na ubinadamu kuwa mtoto wa
mwenzio ni mwanao na baba wa
mwenzio ni baba yako na siyo
baba mkubwa wala mdogo, ni
baba yako mzazi, hapo
tutakapoonesha kizazi hiki na
kijacho. Tofauti na hapo anko
tuking’ang’ania baby, baby,
tutakuja kukosa ushahidi kweli.

FUMANIZI LA AINA YAKE AFUMANIWA AKI DO NA MKE WA MTU LIVE

NI kweli ukistaajabu ya Musa
utayaona ya Firauni! Fumanizi la
aina yake lilitokea juzikati
asubuhi ya saa 2, Mtaa wa
Mbwela, Tandika jijini Dar
ambapo mjamzito aliyejulikana
kwa jina la Semeni alipata
‘kichaa’ cha muda baada ya
kumfumania mumewe, Dullah
akiwa na mwanamke mwingine
chumbani kwao, Risasi Jumamosi
lina kisa kizima.Akisimulia mkasa
huo, Semeni mwenye ujauzito wa
miezi 6 alisema kabla ya tukio
aligombana na mumewe akarudi
kwao kwa muda wa siku mbili
lakini walikuwa wakiwasiliana
mpaka asubuhi ya tukio ambapo
alimpigia simu kumwambia
anafuata nguo kwa vile
anakwenda kliniki.
“Nilipokuwa njiani nilimpigia simu
mume wangu, nikamwambia
nimekaribia, lakini akasema yeye
amekwenda Posta.
“Pamoja na majibu hayo,
niliamua kwenda. Nilipofika
nilikuta mlango umefungwa kwa
ndani, nikampigia simu mume
wangu, akasisitiza hakuna mtu,
yeye yupo Posta.
“Nilichungulia na kuona funguo,
nikajua kuna mtu ila hataki
kunifungulia, hapo wasiwasi
ukazidi kwamba huenda kuna
jambo linaloendelea,” alisema
Semeni.
Mwanamke huyo aliendelea
kuanika kwamba kufuatia hali
hiyo aliwaita majirani ambao
ilibidi wamtishe mtu aliye ndani
kwamba asipofungua watavunja
mlango, ndipo mlango
ukafunguliwa na kumkuta Dullah
akiwa na mwanamke mwingine
chumbani, lakini mumewe huyo
alichoropoka na kukimbia.
“Nilishtuka, nikapiga kelele ya
mshangao kutokana na kitendo
alichokifanya mume wangu,
kumleta hawara mpaka kwenye
chumba tunacholala!
“Sijaamini kilichotokea! Yule ni
mume wangu, amewezaje
kumleta mwanamke ndani ya
chumba tunacholala tena kuna
wapangaji wenzangu
wameshuhudia,” alisema
mwanamke huyo huku akilia
machozi.
Akaendelea: “Mimi hapa
nyumbani siachiwi hela ya kula,
kila siku nakula nyumbani kwetu,
nikijua labda mume wangu hana,
kumbe anamalizia kwa hawara!
Jamani inaniuma sana, kama
hivyo bora amuoe basi tuje tuishi
wote au aniache akae yeye.”
Akizungumza na gazeti hili kwa
uso ‘uliochunwa’, mwanamke
aliyedaiwa kufumaniwa,
Mwanaidi huku akiwa
‘ametaitiwa’ ndani, alijitetea
kuwa hakufahamu kama Dulla
ana mke.
“Mimi aliniambia hana mke wala
mtoto na ndiyo maana nilikubali
kuanzisha uhusiano wa kimapenzi
na yeye si vinginevyo, kama
ningejua nisingekubali kuja, kwa
hiyo siyo kosa langu,” alisema
Mwanaidi.
Baada ya hali kutulia, baba mzazi
wa Dullah ambaye anaishi jirani
aliitwa kuamua ugomvi huo na
kuamuru wote waende nyumbani
kwake ambapo aliagizia gari.
Wawili hao walipofika nyumbani
kwa mzazi huyo walimshusha
Semeni na kumtaka atangulie
ndani, alipoingia tu, nyuma
dereva alitakiwa kuondoka gari
hilo kwa kasi huku Mwanaidi
akiwemo ndani ili kumnusuru.
Baada ya kubaini ‘triki’ hiyo,
Semeni alijirusha chini kwa
hasira na kujigalagaza kisha
kulikimbiza gari hilo bila
mafanikio.

MWANAFUNZI AJICHOMA KISU BAADA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE [2013] KUTOKA

Kijana ambae jina lake halija
famika mpaka sasa,aneishi
mwananyamala dar es salaam
anae semekana kuwa ni
mwanafunzi ambae alimaliza
kidato cha nne mwaka jana yan
elfu 2013 alikutwa amejichoma
kisu shingoni na
kuwahishwa hospital ,huku
chanzo kikisemekana kuwa ni
matokeo yako ya kidato cha
nne,matokeo yake hayakuwa
mazuri maana amefeli kwa kupata
ziro... Tutazidi kuwapa taarifa

Friday, February 21, 2014

KUMBE WASANII WAKIKE WANAOENDA NJE YA BONGO KUFANYA MATANUZI WANAKUWA WAMEFANYA BIASHARA YA KUJIUZA

wanaoenda huko nje sababu
ya kufanya shopping ni uongo
mtupu maana ...(akataja jina
la msanii mkubwa wa kike)
alishawahi kwenda huko tena
alienda kwa ajili ya kigogo
mmoja hapa nchini ambaye
alitaka wakutane huko Dubai
kwa ajili ya mapenzi ndipo
akapata fulsa ya kufanya na
shopping baada ya kupewa
pesa na kigogo huyo" Alisema
rafiki huyo kama kawaida
ilitaka kujua ukweli mzima
upoje inakuwaje wanaenda
nje kufanya hizo shopping na
ni kwa kipato gani
wanachopata maana kila siku
wanalia kuwa wasanii maisha
ni magumu sasa inakuwaje
wanaweza kwenda nje ya nchi
kufanya matanuzi tu?? rafiki
huyo alifunguka na kusema
tena "Ulishawahi kumuona
msaniii gani wa kiume
kaenda kufanya shopping
nje ya nchi?? jibu ni hakuna
na wao ndiyo wanapata
pesa nyingi sana kuliko hao
wa kike. wasanii wa kike
wengi wao wanajiuza kwa
vigogo ndiyo maana
wanapata hiyo jeuri ya
kufanya matanuzi hayo nje
ya nchi"
crew yetu ilizidi kumuuliza
rafiki huyu wa msanii mkubwa
hapa tz kuhusu hilo swala
naye bila hiyana aliendelea
kufunguka "Hapa bongo kuna
vigogo wakubwa sana
wenye pesa zao sasa huwa
wanatafuta wasanii wakike
wenye tamaa kwa ajili ya
kwenda kufanya nao
mapenzi ila vigogo hao
wanaogopa sana mapapalazi
kwahiyo huwa
wanawachukulia kila kitu
kuanzia usafiri pamoja na
malazi katika nchi
watayofikia na lengo likiwa
ni kufanya mapenzi tu"
Ilibidi tumtafute msanii wa
kike ambaye anaweza
kufunguka juu ya suala hili
ndipo tulipompata Snura na
hivi ndivyo alivyofunguka
baada ya kumuuliza "Ni kweli
wasanii wengi wa kike
wanatabia hiyo na wengi
wao wanajiuza kweli,
ninawafahamu kadhaa ila
siwezi kuwataja" alimaliza
snura kwa kusema hayo

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA!

Majira ya saa nane mchana siku
ya leo, hatimaye matokeo ya
kidato cha nne 2013
yametangazwa baada ya
kusubiriwa kwa hamu na wadau
kwa muda mrefu sana. Jedwali
hili hapa chini ni summary tu ya
matokeo hayo kwa ujumla.
Hizi ndio shule 10 bora matokeo
kidato cha nne 2013:
1. St.Francis Girls (Mbeya)
2. Marian Boys (Pwani)
3. Feza Girls (Dar-es-salaam)
4. Precious Blood (Arusha)
5. Canossa (Dar-es-salaam)
6. Marian Girls (Pwani)
7. Anwarite Girls (Kilimanjaro)
8. Abbey (Mtwara)
9. Rosmini (Tanga)
10. DonBosco Seminary (Iringa)
Hawa ndio wanafunzi 10 bora
matokeo kidato cha nne 2013:
1. Robina S Nicholaus (Marian
Girls - Pwani)
2. Magreth Kakoko (St. Francis
Girls - Mbeya)
3. Joyceline Leonard Marealle
(Canossa - Dar-es-salaam)
4. Sarafina W. Mariki (Marian
Girls - Pwani)
5. Abby T Sembuche (Marian
Girls - Pwani)
6. Sunday Mrutu (Anne Marie -
Dar-es-salaam))
7. Nelson Rugola Anthony
(Kaizirege - Kagera)
8. Emmanuel Mihuba Gregory
(Kaizirege - Kagera)
9. Janeth Urassa (Marian Girls -
Pwani)
10. Angel Ngulumbi (St. Francis
Girls - Mbeya)
Matokeo yatapatikana muda sio
mrefu kuanzia sasa kupitia tovuti
zifuatazo:
http://www.necta.go.tz/
http://moe.go.tz/
http://tanzania.go.tz/
http://pmoralg.go.tz/
http://moez.go.tz/
Pia, matokeo yanaweza
kupatikana kwa njia ya ujumbe
mfupi wa maneno (SMS) kupitia
namba 15311. Jinsi ya kutuma
ujumbe, Andika:
MatokeoXNamba ya
kituoXNamba ya Mtahiniwa
Mfano: matokeoxS0101x0503

Thursday, February 20, 2014

HUYU NDO MZUNGU BODABODA ALIYE RUDISHWA KWAO POLAND NA SERIKALI

baadhi picha anaonekana akiwa katika kituo akisubiria abiria.
kweli maisha popote

Wednesday, February 19, 2014

KOMANDO JIDE SASA AJIFUA KWA KARATE

Mwanadada Jide kwa sasa yupo
kwenye mazoezi ya Karate ili
kuuweka mwili wake uwe vizuri
na ujijenge kwa lolote litakalo
kuwa lakijinga mbele yake ili
akabiliane nalo. Jide akitumia
account yake ya Facebook
ametupia picha hizi ambazo ziko
hapa akiwa na vazi jipyaaaaaaaa
kabisa tayari kwa kuyamudu
mazoezi hayo.

Tuesday, February 18, 2014

P FUNK MAJANI

P Funk Majani amewapa makavu
watu wanaochonga kuhusu
maendeleo yake hususani wale
wote ambao wanapiga majungu
kuwa mkali huyo amepotezwa na
vijana wadogo kwenye industry
ya mziki.
“Kuna watoto wadogo siku hizi
wanakurupuka wanajiona wao
ndio wao, juzi kati nikiwa kwenye
club moja nasikia kiproducer
kinachonga kuhusu mimi
kenyewe kana sijui nyimbo moja
au tatu zimehit mimi nina
nyimbo zaidi ya 100 ambazo
zimehit na hadi akina Mhe Mkapa
enzi hizo, wametukubali we
utaniambia nini” P funk alinena.
Majani amefunguka kuwa kuna
watu wanamtafuta chuki ili
kumpachika skendo akitolea
mfano msanii wa kizazi kipya Ney
wa Mitego kuwa haelewi kitendo
cha rapper huyo kumtukana
kwenye nyimbo yake kulikua na
lengo gani kwasababu msanii
huyo hamkaribii hata kidogo kwa
level zake.

JUMA NATURE

Msanii mkongwe wa muziki wa
kizazi kipya hapa bongo Juma
Kasimu Ali Kiroboto ama Juma
nature ameamua kuondoa utata
alioibuka juu ya kipande cha
mistari katika wimbo wake mpya
kinachotaja jina linalodhaniwa
kuwa ni la Diamond.
Katika mahojiano na kituo cha Rfa
msanii huyu amesema hilo jina la
Dada mondi ni la msanii ambaye
ni underground na kuwa anapenda
misifa hivyo akaamua kumchana
na sivyo kama watu wanavyodhani
kwa ni Diamond.

Monday, February 17, 2014

YOUNG KILLER AKUTANA NA MAWITA ANYANG‘ANYWA PENSI ALIYOKUWA AMEVAA YENYE RANGI YA JESHI

Young killer juzi kati
amenyang’anywa pensi aliyokua
amevaa…pensi hiyo yenye rangi
za kijeshi alivuliwa huko mwanza
kipindi akipita karibu na kambi
moja ya jeshi huko jijini
mwanza.. young killer alipost
picha hii kisha kuandika maneno
haya mtandaoni....
Jeshi..letu la tanzania .na
wasifu..xana wako silias xana na
kazi yao...jana
jion..wamefanikiwa kunivua hii
pensi yao..ambayo
mim..niliipenda kwa dhat kuliko
nguo zote nilizo nazo
nyumbani..R.I.P..pensi yangu..
za idi msikilize hapa chini...

WASTARA JUMA APATA AJALI MBAYA YA GARI

MAJANGA! Siku chache baada ya
hivi karibuni kudaiwa kunywa
sumu, staa mkubwa wa sinema
Bongo, Wastara Juma amepata
tena ajali mbaya.Habari za
uhakika zilizolifikia gazeti namba
wani la burudani Bongo, Ijumaa
Wikienda mwishoni mwa wiki
iliyopita zilieleza kuwa siku ya
tukio Wastara alitoka nyumbani
kwake Tabata-Bima, Dar na gari
lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili
ya kwenda kununua umeme.
Akizungumzia tukio hilo kwa
masikitiko, Wastara aliliambia
gazeti hili kuwa kabla ya kufika
kwenye kituo cha kununulia
umeme (Luku) alikutana na lori
kubwa lililokuwa kwenye mwendo
kasi huku likiwa limewasha taa
fulu.
Alisema kuwa alijaribu kulikwepa
lakini lilimsukuma na kujikuta
akiingia mtaroni kutokana na
barabara kuwa nyembamba
ambapo aliumia sehemu za
kichwani na mguuni kwa ndani.
Wastara alisema baada ya hapo
alikimbizwa katika Hospitali ya
TMJ, Dar ambapo alisafishwa
majeraha (dressing) kisha
akapatiwa matibabu na baadaye
aliruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nimenusurika kifo, namshukuru
sana Mungu kwani ajali ilikuwa
mbaya nilihamishwa kwenye siti
niliyokuwa nimekaa na kurushwa
kwenye siti nyingine huku
nikijigonga na kuumia kichwani.
“Pia gari langu limeharibika sana,
kioo chote kimevunjika, sielewi
kwa nini haya yote yananitokea.
“Namuomba Mungu anisaidie
maana naona mambo
yanakwenda ndivyo sivyo na kwa
nguvu zangu mwenyewe
siwezi,”alisema Wastara.
Hata hivyo, Wastara kwa sasa
anaendelea vizuri japokuwa bado
anaumwa kichwa na mguu.
Wastara ameshapata ajali mara
kadhaa ikiwemo ile ya pikipiki
aliyopata mwaka 2008 akiwa na
aliyekuwa mumewe, Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi
akatwe mguu wa kulia. Pia
aliwahi kupata nyingine ya gari
akiwa na Sajuki.
Kwa mujibu wa watu wa karibu
wa Wastara, kuna watu
wanamtakia mabaya ili amfuate
Sajuki aliyefariki Januari 2, mwaka
jana.

JAMANI HIZI NI DALILI ZA NINI ? DUME LA VAA NYWELE BANDIA NA KUTINDA NYUSI

jamani tunakwenda wapi tazama kijana huyu alivyo weka nywele za kike pia ametinda nyusi anada eti anakwenda na wakati.

SIKILIZA SABABU ILIYOMFANYA RICH MAVOKO KUKIMBIA NA MASHUKA YA HOTELINI

Week end iliyopita Mavoko na
Shettah walienda kufanya show
Mtwara miongoni mwa vitu
vilivyotokea kwenye hotel
waliyolala ni kuhusu kuondoka
na mashuka ya hiyo hotel.
bofya hapa kwa taarifa hizo hapa chini.... ...  ..  

HAPA PALIKUWA HAPATOSHI TAZAMA PICHA ALI KIBA ALIVYO WAPAGAWISHA MASHA BIKI WAKE SIKU YA VALENTNES DAY

Siku ya Valentines Day na
msanii kutoka Bongo Ally Kiba
alikuwa anashow pande za
Muscat na show aliyopiga
unaambiwa haijawahi tokea
kwa msanii yoyote aliyeenda
kufunika kama Ally Kiba jana.
Kila wimbo aliokuwa akiuimba
watu walikuwa wanashangilia
na unaambiwa ilikuwa ni Live
Band tu.

Sunday, February 16, 2014

LIL KIM ATARAJIA KUITWA MAMA SIKU ZIJAZO KUTOKANA NA HALI ALIYOKUWA NAYO KWAKIPINDI HIKI

Lil Kim karibuni atakuwa
mama
Rapper kutoka Marekani
amewashangaza karibu kila
mmoja mara baada ya
kuwasili kwenye Blonds Fall
2014 fashion presentation siku
ya Jumatano 12 February
2014, akionyesha accessory
yake mpya "Mimba"
Lil Kim, 39 ,aliwasili katika
event hiyo akiwa na nguo
ndefu ya velvet nyeusi, koti la
manyoya la pink na buti za
Hello Kitty .

Baadae Lil Kim ali-perform
kwenye after party na kutangaza
ujauzito wake

“I’m a mom, but I can turn it
up a little! I’m still going to
work. I’m still going to be
hardcore, the baby has made
me even more of a beast!” she
said while rubbing her bump.

BEN POL-JIKUBALI LYRICS

Verse1;
Unaweza kuwa Doctor,
unaweza kuwa Star
Unataka kuwa Linah, unaweza
kuwa Shaa
Kipaji Mali yako, Elimu Ngao
yako
Usiache jambo Kati kwenye
maisha yako
Unaweza kuwa Diamond,
unaweza kuwa Jay
Unaweza kuwa JB, unaweza
kuwa Ray
Mi Nakuasa it's your time,
Huwezi kuwa chini you've got
somethin' special
Unampenda Lady Jay dee
unamzimia Zitto
Trust me iko siku utatimiza
ndoto yako
You can be a Boss, you can be
a Lawyer
You can be the President
You'll be successful
Chorus;
Wakati wako ndio leo (leo)
Kutimiza malengo yako,
Nakusihi Anza sasa (sasa)
Jishughulishe utapata (rudia
mara mbili)
Verse 2;
Utavunja vunja miamba,
hamisha milima
Vikwazo lazima nawe usirudi
nyuma
You'll be a hero, you can be
the best
You can be a leader (dedicate
yourself)
Tanzania ni yako, penda watu
wako
Kuwa mfano bora kwenye
jamii yako
Star Kama AY , kufika alipo FA
Inawezekana if you work hard
in it
Na utafika mbali utazame
ulikotoka
Mbunifu mwenye hadhi kama
Hadija Mwanamboka
Unaweza kuwa rubani,
unaweza Hakimu
Unataka kuwa Salama,
unaweza kuwa Hasheem'
(Rudia chorus)
(Bridge)
You can be a champion
(Jikubali)
You can be a teacher
(Jikubali)
You can be a leader (Jikubali)
You can be a Preacher
(Jikubali)

BRAND NEW SINGLE: Penzi -Quick Rocka feat Ben Pol

Brand new single: Penzi -
Quick Rocka feat Ben Pol
"Asilimia 70 ya wimbo huu
ameuandika Ben Pol pamoja na
melody," amesema Quick Rocka
wakati anautambulisha wimbo
huu. akiwa amemshirikisha Ben
Pol huyo huyo Quick amesema
wimbo huu hasa unawahusu wale
ambao wanapendwa lakini
wanakuwa hawawajali
wanaowapenda.

http://www.hulkshare.com/Yuskisskisiba/penzi-by-quick

http://www.hulkshare.com/kyarwenda/penzi-by-quick

CHADEMA YA TISHIA KUSUSIA BUNGE LA KATIBA

8WAKATI keshokutwa Bunge
Maalum la Katiba linaanza
kukutana mjini Dodoma, Chama
cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimesema huenda
kikasusia Bunge Maalum la Katiba
iwapo litaendeshwa kwa kufuata
matakwa ya chama cha siasa na
siyo ya wananchi.

JK AWATAKA WANACHAMA WAKE WAVUNJE UKINMYA ZIDI YA KUONEWA KWAO NA WANACHAMA PINZANI

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya
Kikwete amewataka wanachama
wake kuacha unyonge na kujibu
mapigo ya wapinzani hasa wale
ambao wanaendesha siasa za
vurugu katika kampeni za chaguzi
mbalimbali nchini.
Rais Kikwete amesema kuwa
uvumilivu una ukomo, na kwamba
sasa wanachama wa CCM hawana
budi kuacha unyonge, kutokana na
siasa hizo za vurugu
zinazoendeshwa na vyama vya
upinzani.
Aliyasema hayo jana mjini hapa
wakati akifungua kikao cha
kawaida cha Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya CCM
kitakachokutana kwa siku mbili
chini ya uenyekiti wake, ambacho
ajenda kuu ni kuzungumzia Bunge
Maalumu la Katiba.
“Tumelizungumzia hili katika
Kamati Kuu, tumekubaliana kuacha
unyonge (makofi). Ndio watu
wamelisema hili katika Kamati
Kuu, tumesema jamani
tumekubaliana kuacha unyonge,”
alisema Rais Kikwete ambaye
wakati anafungua kikao hicho
waandishi wa habari walikuwamo,
na akaongeza: “Wacha wakaseme
(waandishi wa habari), ndio
tumekubaliana kuacha unyonge.
Kabisa. Hata kama leo katika
taarifa za habari, zisiwekwe habari
nyingine, msikike ninyi tu.
Uvumilivu una ukomo wake.”
Mwenyekiti huyo wa CCM alisema
wamefikia hatua hiyo kwa sababu
yanayotokea yanasikitisha sana na
akatoa mfano wa matukio kadhaa
ya uvunjifu wa amani katika
kampeni katika maeneo ya Igunga
mkoani Tabora na Kahama mkoani
Shinyanga.
“Maana tunashindana na wenzetu
wagomvi maana wao ugomvi ndio
sehemu ya mwongozo wa kufanya
kazi ya siasa. Maana pale Kahama
kijana wamemtoa macho kwa
bisibisi. Acheni unyonge (makofi).
“Nasema kwa kweli kwa sababu
yanayotokea yanasikitisha. Pale
Igunga kijana yule wamemmwagia
tindikali, pale Kahama kijana
wamemtoa macho kwa bisibisi.
Tuache unyonge,” alisisitiza Rais
Kikwete huku akishinikizwa kwa
shangwe za CCM Oyee, Mapinduzi
Daima.
Ingawa Rais Kikwete hakutaja
chama, Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimekuwa
kikihusishwa na vurugu za
uchaguzi katika maeneo
mbalimbali yakiwamo ya Igunga
na Kahama katika uchaguzi mdogo
wa madiwani uliofanyika hivi
karibuni na pia katika chaguzi
ndogo za ubunge.

KEEP SWAGG‘Z ON CAMERA

SASA UNAWEZA KUTUMA PICHA YAKO KATIKA UKURASA HUU KUINGIA KATIKA KUONESHA NA KUTANGAZA MITINDO MBALIMBALI YA MAVAZI,UREMBO NA MAPOZI KIBAO NDANI YA  PICHA.
SHIRIKI SASA BUREEEEE.....

KEEP SWAGG‘Z ON CAMERA
KAMA UNATAKA KUTUTUMIA  PICHA. TUMA KWA Whatsapp
Namba 0655323305

CHEKI NGUO YENYE TAA KWENYE MAKALIO

NGUO HII IME WASHANGAZA WATU WENGI SANA PINDI MWANA DADA  ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA  LA RUNNA ALIPO KUWA AMEVAA VAZI HILI.
UNAAMBIWA HII NI MAALUM
KWA AJILI YA KUPUNGUZA
AJALI...NIAJE MDAU WAONA
INA TIJA KWELI AU NI KITUKO
TU DIZAINI FLANI MAJUU
HAMNAZO...