Mwandishi Wetu
AMA kweli dunia hadaa,
ulimwengu shujaa! Kumeibuka
mchezo mchafu,
kuna Watanzania wanawachukua
warembo nchini na kuwapeleka
China kwa ahadi kwamba
wanakwenda kufanya kazi saluni,
wakifika kule wanawanyang’anya
paspoti na kuwauza kwa
wanaume (ukahaba), sasa
yamemkuta Mbongo aitwaye
Sabrina au Habiba, Ijumaa
Wikienda lina mkasa wa
kusikitisha.
Habari za uhakika kutoka kwa
chanzo chetu nchini humo
zilisema kuwa, Sabrina (24),
alifariki dunia Alhamisi iliyopita
kufuatia kubakwa na wanaume
watano, raia wa Nigeria ambao
wamo nchini humo kibiashara.
Tukio hilo lilijiri kwenye hoteli
moja iliyopo kwenye Mji wa
Guangzhou ambao umejaa
wageni wengi, wakiwemo
Watanzania.
SIKU YA TUKIO
Rafiki wa karibu wa Sabrina,
Saada alisema siku ya tukio,
marehemu akiwa katika harakati
zake za kutafuta wateja alikutana
na Mnigeria mmoja ambaye
walipatana kulala wote kwa usiku
mzima.
“Kumbe yule Mnaigeria alikuwa
na wenzake wanne. Usiku
walimwingilia wote kwa nguvu
kwa kumbaka mpaka akapoteza
maisha palepale. Ni ukatili
mkubwa.
“Wale watu walipogundua
Sabrina amekufa waliuchukua
mwili wake na kuutupa chini
kutoka ghorofa ya tano,” alisema
rafiki huyo.
MAITI YAKUTWA HAINA FIGO,
MOYO
Habari zaidi zilidai kuwa mpaka
juzi (Jumamosi) madaktari
waliokuwa wakiuchunguza mwili
wa Sabrina waligundua hauna
figo na moyo, jambo linalozidi
kuzua hofu juu ya muaji yake.
NI BIASHARA ILIYOIBUKA CHINA?
Ilidaiwa kuwa nchini China
imeibuka biashara ya viungo
mbalimbali vya binadamu
ambapo ili vipatikane ni lazima
mwenye viungo hivyo auawe kwa
njia yoyote.
SABRINA AFA, MGANDA APOTEA
Mtoa habari wetu alisema wakati
Wabongo wakiwa kwenye
maombolezo ya kifo cha
Mtanzania huyo, mrembo
mwingine raia wa Uganda, nchi
ambayo imo ndani ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki amepotea katika
mazingira ya kutatanisha nchini
humo.
Baadhi ya watu wana wasiwasi
kuwa kupotea kwa msichana
huyo kunahusiana na kushamiri
kwa biashara ya viungo vya
binadamu.
SABRINA ALIKWENDAJE CHINA?
Mwezi Julai, mwaka jana, Sabrina
alikwenda nchini humo
akidanganywa na mwanamke
mmoja kwamba atapata kazi
kwenye saluni ya wanawake lakini
baada ya kufika alijikuta
akiingizwa kwenye biashara ya
ukahaba bila ridhaa yake mpaka
alipokutwa na mkasa huo
uliopoteza maisha yake.
TAHADHARI KWA WAREMBO
WANAOKWENDA CHINA KUFANYA
KAZI SALUNI
Imebainika kuwa, kumeibuka
wimbi la Wabongo wanaofanya
‘uwakala’ wa kuwachukua
wasichana wa Kitanzania kwa
kuwadanganya kwamba
wanakwenda kufanya kazi za
saluni nchini humo.
Mara baada ya kufika, wasichana
hao hunyang’anywa paspoti ili
washindwe kuondoka nchini
humo na kushinikizwa kujiuza
(ukahaba) huku waliowapeleka
wakipokea fedha kutoka kwa
wateja.
KUIKOMBOA PASPOTI
Habari zilisema kuwa mhusika
hurejeshewa paspoti yake baada
ya malipo yake kwa ‘wakala’
kufikia dola za Marekani 8,000
(kama shilingi milioni 12), ndipo
huachiwa ‘huru’ kuendelea na
maisha yake.
Wengi wakishaachiwa hushindwa
kurejea Bongo na kujikuta
wakiendelea kuuza miili katika
mahoteli na klabu huku
wakikutana na majanga
mbalimbali.
MASOGANGE, KAJALA NA DIDA
Watanzania waishio nchini humo
wamewatahadharisha mastaa wa
Bongo, wakiwemo Mtangazaji wa
Radio TimesFM, Khadija Shaibu
‘Dida’, msanii wa filamu Kajala
Masanja na Video Queen Agnes
Gerald ‘Masogange’ ambao
hupenda kwenda nchini humo
kwa shughuli zao, kutokubali
kuwa karibu na mawakala wa
kuchukua wasichana Bongo kwa
kuwadanganyia kazi ya saluni
kwani wanaweza kujikuta pabaya
siku moja.
DIDA
Ijumaa Wikienda lilimsaka Dida
siku ya Jumamosi iliyopita na
kumuuliza kuhusu kuwepo kwa
mawakala hao ambapo alikiri
kusikia huku akisema warembo
wenyewe wanapaswa kuwa
macho na udanganyifu huo.
“Najua wapo Wabongo
wanaofanya shughuli hiyo, si
China tu hata India, unapelekwa
kwa ahadi ya kazi ya saluni,
ukifika hamna cha saluni wala
nini? Warembo wawe makini
jamani, nenda China kama una
uwezo wako mwenyewe kufanya
‘shoping’ lakini si kupelekwa,”
alisema Dida.
BALOZI WA TANZANIA-CHINA
Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta
Balozi wa Tanzania nchini China,
Luteni Jenerali Mstaafu
Abdulrahman Shimbo ili
azungumze lolote kuhusu tukio la
Sabrina, lakini simu yake
ilionekana kutokuwa hewani kwa
muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment