ads

Thursday, May 8, 2014

JUA SABABU 10 ZINAZO SABABISHA MAPENZI KUPUNGUA

Habari zenu wadau wa blog hii,naamini umzima na unafurahia darasa hili la watu wazima,Hebu leo tuangazie mambo 10 yanayo sababisha mapenzi kupungua

Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.


Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-

1.       UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.

2.       USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.


Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.

3.       ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi. 

Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo,  Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.

4.       DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.

Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri  au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja Suala La Ndoa/Kuishi Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa Mwanamke Kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.