ads

Friday, February 14, 2014

UTAMBUE UJIO MPYA WA MSANII MB DOG NDANI YA GAME LA MUZIKI WA BONGO

MKALI wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Mbwana
Mohammed maarufu kama
Mb Dogg, yupo kwenye
mipango ya kuachia wimbo
wake mpya unaokwenda kwa
jina la Baby mbona
umenuna?
Mb Dogg pichani, wimbo
wake mpya wa 'Baby Mbona
Umenuna' utakuwa balaa na
unatarajiwa kumuweka tena
kileleni.
Wimbo huo umerekodiwa
katika Studio za Maccopa,
ambapo unatarajiwa
kurudisha makali na heshima
ya msanii huyo aliyewahi
kuwika katika tasnia hiyo.
Akizungumza jana jijini Dar
es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Qs Mhonda J
Entertainment, Joseph
Mhonda, alisema kwamba
wimbo huo ni moto wa
kuotea mbali ambao kwa
kiasi kikubwa utamuweka
juu zaidi.
Alisema kwamba Mb Dogg ni
msanii aliyejichimbia kwa
muda mrefu akiwa na
mahitaji ya kurudi kwenye
nafasi zake za juu alipokuwa
awali.
“Sisi kama Kampuni
tunaofanya kazi na Mb Dogg
tunaamini kabisa huu ni
wakati wake wa kurudi tena
kileleni ili aendeleze makali
yake ya awali.
“Baby Mbona umenuna ni
wimbo ambao kwa hakika
utadhihirisha ubora wa
mwimbaji huyu wa Latifa na
nyinginezo zilizomuweka
kileleni,” alisema.
Mb Dogg anatokea katika
kampuni hiyo kwa sasa,
akiwa sambamba na Nay wa
Mitego anayetamba na
wimbo wa Muziki Gani,
aliyeimba na Diamond.

Mwigizaji na shoga maarufu wa Nollywood Nigeria afariki ghafla akimegwa!

Mwigizaji maarufu Charles
Warren ambaye ni shoga
anayeigiza sinema katika
tasnia ya sinema ya Nollywood
nchini Nigeria amefariki ghafla
alhamisi iliyopita majira ya
usiku katika Hospitali moja
jijini Lagos nchini Nigeria.
Charles Warren alifariki ghafla
wakati akiifanya mapenzi
(akimegwa) na mwenzake
aliyetajwa kwa jina la Ajah
ambapo ghafla alianza kulalamika
maumivu ya kiuno na baadaye
maumivu hayo yakahamia
mgongoni ambapo baadaye
alipata haja kubwa mara nne
ndani ya muda wa dakika 30.
Baadaye maumivu hayo
yalihamia kifuani ambapo ilibidi
awahishwe katika hospitali ya
Safeway kwa matibabu zaidi.
Rafiki yake aitwaye Ajah ambaye
ndiye waliyekuwa wakifanya naye
mapenzi alijaribu bila mafanikio
kumfanyia masaji kifuani ili
kumpunguzia maumivu lakini
haikusaidia, Warren alifariki
dunia usiku huo huo.
RIP Charles Warren.

Monday, February 10, 2014

ROSE MUHANDO MBARONI KWA UTAPELI

STAA wa nyimbo za Injili Bongo,
Rose Muhando yamemkuta ya
kumkuta ambapo Ijumaa iliyopita
alishikiliwa na Polisi wa Kituo cha
Msimbazi jijini Dar es Salaam
kwa madai ya kuingia mitini na
shilingi milioni 6 alizolipwa kwa
ajili ya kwenda kufanya shoo ya
kiroho, Mombasa, Kenya
Novemba 3, 2013 lakini
hakutokea. Kwa mujibu wa
chanzo chetu, Rose alidakwa jijini
Dar es Salaam saa sita mchana
huku mlalamikaji wake akiwa ni
mtu aliyejulikana kwa jina la
Nathan Wami.
Nathan amewahi kuwa meneja
wa kazi za Rose Muhando. Kwa
sasa Rose anaratibiwa na
Kampuni ya Sony.
MADAI YA JALADA LA KESI
Kwa mujibu wa chanzo, jalada la
kesi hiyo lilifunguliwa Dodoma
likisomeka; DOM/RB/1129/2014
KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA
UDANGANYIFU.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Rose
aliachiwa kwa dhamana akitakiwa
kurudi kituoni hapo Februari 8,
2014 huku mkononi akiwa
ameshika kiasi hicho cha fedha
kwa ajili ya kumlipa mlalamikaji
huyo.
WIKIENDA LATINGA POLISI
MSIMBAZI
Baada ya kuinyaka nyeti hiyo,
Ijumaa Wikienda lilipiga hodi
kituoni hapo na kuulizia kama ni
kweli nyota huyo wa wimbo wa
Utamu wa Yesu alishikiliwa.
“Sisi si wasemaji wakuu wa polisi,
hatuna mamlaka hayo. Hatuwezi
kusema ni kweli au si kweli,”
afande mmoja alilijibu gazeti hili.
MADAI NYUMA YA PAZIA
Wakati madai ya Rose yakiwa
hayo, nyuma ya pazia kuna
mlolongo wa matukio ya
kushangaza kati ya mwimbaji
huyo na Nathan.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja,
Rose amekuwa akiingia kwenye
madai ya kupokea fedha za shoo
na kutokwenda lakini Nathan
akielekezewa lawama zote.
PESA APOKEE MENEJA, LAWAMA
ABEBESHWE ROSE
“Jamani mimi nataka kuwaambia
ukweli, Rose hahusiki na hiyo
tabia. Wengi wanasema ana
mchezo wa kuchukua fedha za
watu halafu haendi kwenye tukio
lakini ukweli si huo,” kilisema
chanzo hicho.
Wikienda: “Ukweli ni upi? Funguka
basi.”
Chanzo: “Ukweli ni kwamba,
Nathan amekuwa akimnyanyasa
sana Rose kwa muda wote
aliokuwa meneja wake.
“Ilifika mahali, Nathan ndiye
alikuwa akipokea pesa kutoka
kwa watu wanaomhitaji Rose bila
kuwasiliana na mwenyewe.
Wakati mwingine Rose hajulishwi
mapema.
“Siku akiambiwa, pengine
anaumwa au yupo mbali na eneo
la tukio, sasa hapo waandaaji
wanamsema Rose kwamba
amechukua fedha na kuingia
mitini,” chanzo kilizidi kuweka
wazi.
ROSE HANA CHA KUFANYA
Kwa mujibu wa chanzo, hali hiyo
imekuwa ikimsumbua sana Rose
kwani ni kweli wengi wanaamini
hivyo lakini ukweli ni kwamba
anasingiziwa tu, Rose hawezi
kupokea fedha halafu asiende
kuimba ila kwa sababu Nathan ni
meneja wake aliyemtoa kisanii
anajikuta hana la kufanya.
“Mbona kwenye matamasha ya
Pasaka na Krismasi
yanayoandaliwa na Msama
Promotion hatujawahi kusikia
Rose kaingia mitini? Ni kwa
sababu Msama mwenyewe
anawasiliana naye moja kwa
moja,” kiliendelea chanzo.
NATHAN ALIISHI NA ROSE KWA
UBABE
Ikazidi kudaiwa na chanzo chetu
kwamba katika kipindi chote,
Nathan amekuwa akiishi na Rose
kwa ubabe wa hali ya juu, jambo
ambalo lilimuathiri Rose
kisaikolojia bila kujijua.
“Kuna mengi sana, tena yale ya
ndani zaidi, sipendi kuyasema
lakini Nathan mwenyewe
anayajua, siku ikifika nitayalipua
kama atapinga,” kilisema chanzo.
ROSE MUHANDO HUYU HAPA
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Rose
kwa lengo la kutaka kumsikia
atakachokisema juu ya madai
yote hayo kuhusu yeye na
Nathan, lakini zaidi ya yote tukio
la kuwekwa mahabusu ya
Msimbazi Polisi, msikie:
“Kusema ule ukweli mimi
namwachia Mungu, yeye anajua
ukweli uko wapi na uongo uko
wapi!”
NATHAN SASA
Baada ya hapo, gazeti hili
lilimtafuta Nathan Wami na
kumsomea mashitaka yote.
Nathan: “Hayo madai si ya kweli.
Kama kasema yeye siyo kweli.
Nimeishi na Rose karibu miaka
kumi na mbili, nilikuwa
namchukulia kama mtoto wangu.
“Nimekuwa nikiona kwenye
magazeti kwamba eti alisaidiwa
na mfuko wa kanisa wakati mimi
ndiye niliyemtoa.”
Wikienda: “Kwa hiyo madai
kwamba umekuwa ukiishi naye
kibabe, hukuwa unamtendea haki
si ya kweli?”
Nathan: “Si ya kweli hata kidogo.”
MSAMA ANAMLIPA NANI?
Gazeti hili liliwasiliana na
muandaaji wa matamasha ya
Pasaka na Krismasi, Alex Msama
kuhusu malipo ya Rose
Muhando.
Msama: “Mimi huwa namalizana
na Rose.”
Wikienda: “Kuna mwaka umewahi
kumlipa pesa halafu hakutokea
kwenye tamasha lako?”
Msama: “Hapana, hata Tamasha
la Pasaka mwaka huu atakuwepo
panapo uzima maana
tumeshamalizana.”
KUTOKA KAMPUNI YA SONY
Habari zilizopatikana kutoka
Kampuni ya Sony ambayo
inamratibu Rose kwa sasa,
zinasema kuwa wakati wa kuingia
makubaliano na nyota huyo
walikutana na masuala hayo ya
madeni lakini walipofanya
uchunguzi wakagundua mambo
ambayo hawakutaka kuyaweka
wazi lakini kimsingi
walimhurumia Rose.
“Ila mabosi wa Sony waliamua
kuwa yale madeni yaliyopita
watayalipa wao, yale ambayo
tarehe za Rose kuimba bado,
wamemwambia akaimbe ili
kumalizana na wahusika,”
kilisema chanzo hicho na kuomba
kutotajwa jina gazetini.
-GPL

AIBU SHULE YA MSINGI JIJINI DAR,WANAFUNZI WAKAA CHINI

Aibu! Shule ya Msingi Jijini
Dar, Wanafunzi wakaa chini
huku waalimu wakitumia
Khanga kama Majamvi.
Shule ya Msingi Mtambani
iliyoko Kinondoni jijini Dar es
Saalam, haina samani hali
inayosababisha wanafunzi kukaa
chini, wakati walimu
wanalazimika kutandaza khanga
wanazokalia chini ya miti.
“Shule hii ina upungufu wa
madawati, nusu ya wanafunzi
wanakaa chini, hatuna ofisi za
kutosha za walimu wale wasio
na nafasi wanakaa chini ya miti”,
alisema Mwalimu Mkuu
Emmanuel Munisi.
Aliongeza kuwa tatizo hilo
linawalazimisha wengine
kutandika khanga chini ya miti ili
kufanya kazi kwa sababu ya
ukosefu wa meza za kufanyia kazi
na kwamba mvua inaponyesha
wanalazimika kujikusanya pamoja
na wanafunzi madarasani,
alisema Munisi.
Shule ya Mtambani iko taabani
wakati serikali ilipata chenji ya
rada ya shilingi bilioni 43 ambayo
ilielezwa kuwa pamoja na
kununua vitabu mashuleni pia
itawezesha upatikanaji wa
madawati.
Serikali ya Uingereza ilirudisha
fedha hizo kuanzia mwaka jana
na kwamba jukumu la kununua
vifaa hivyo liliachwa kwa Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, ambayo
inasimamia shule za serikali za
msingi na sekondari.
Shule hiyo ina walimu 41 na
wanafunzi 1,830 inakabiliwa na
uhaba wa madawati, viti na
meza za walimu kwa mujibu wa
Munisi. Aliiambia NIPASHE
Jumamosi kuwa mazingira
mabovu ya shule hiyo ni pamoja
na upungufu wa vyoo, ukosefu
wa sakafu madarasani badala
yake madarasa yana mahandaki
na vumbi kila wakati. Akifafanua,
alisema kuwa shule hiyo
ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa na
wanafunzi 77 na ofisi moja
ndongo kwa ajili ya walimu. Hata
hivyo, kwa sasa ina wanafunzi
1,830 wa kike 917, wavulana 913
na walimu 41.
Alisema hakuna maji safi ya
kunywa na wanafunzi wengi
wanakabiliwa na matatizo ya njaa
yanayosababisha kudondoka
mara kwa mara.
Alieleza kuwa wastani wa
kuanguka ni kati ya watoto
watano na zaidi ambao hutibiwa
kwa kuwekewa drip za kuongeza
maji na sukari mwilini.
Madaktari wanasema tatizo ni
ukosefu wa chakula na nguvu
mwilini kwa hiyo
wanapotundikiwa drip wanapona.
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa
Mtambani, Steven Ngonye,
akizungumzia tatizo hilo alisema
litashughulikiwa pamoja na
upatikanaji wa maji na ukarabati
wa shule hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya
Mtambani Maji Safi Sharifu,
alisema serikali inalitambua
tatizo hilo na imetenga bajeti ya
Sh. milioni 108 kwa ajili ya
madawati na ukarabati wa
vyumba vya madarasa na
kwamba hadi sasa madawati 50
yameshapelekwa shuleni hapo.
Akifafanua zaidi alisema kuna
mpango wa kuongeza vyumba
vya madarasa mawili pamoja na
kufikisha maji safi kazi
itakayogharimu Sh. milioni 20.
CHANZO: NIPASHE

AY AFUNGUKA JUU YA YA UZUSHI WAWATU KUSU JAGUAR

Msanii wa HipHop kutoka
Tanzania, Ambwene Yesaya
amekanusha uvumi uliokuwa
umezagaa nchini Kenya wa
kumuandikia baadhi ya nyimbo
mkali wa Kioo kutoka Kenya,
Jaguar.
Katika mahojiano aliyofanyiwa
nchini Kenya alikokuwa ameenda
hivi karibuni, AY amesema hajawai
kumuandikia wimbo wowote
Jaguar na hata wimbo wao
‘Nimetoka Mbali’ kila mtu aliandika
mashairi yake.
“Jaguar ni mmoja wa marafiki
zangu. Tumefanya kazi pamoja na
hakuna ukweli wowote kuhusiana
na tetesi za mimi kumuandikia
mashairi ukizingatia amekuwepo
kwa muda mrefu kwenye gemu ya
muziki hivyo kumfanya kuwa
miongoni mwa wasanii wenye
uzoefu wa kutosha na kufanya
vizuri hata ukitazama ngoma
niliyowahi kufanya nae ya
Nimetoka Mbali, kila mmoja wetu
aliandika mashairi yake kivyake
hivyo huna haja ya kubisha kwa
uwezo mkubwa alionao na naamini
ni ushahidi tosha,” alisema.
Pia AY amepinga muziki wake
kuathiriwa na Diamond kwakuwa
kila mtu ana malengo yake katika
muziki wake.
“Kila msanii ana mipango na
mikakati yake ya kufikia malengo
aliyojiwekea, sipo kujilinganisha na
mtu yoyote, ushindani wangu ni
kwa yule anayetaka kujaribu
kutengeneza mkwanja mkubwa
kushinda wangu, huo ndio
ushindani wa kweli, hata hivyo
siwezi kuwa juu milele.”

BABU AYUBU AFUKUNGA YA MOYONI KUHUSU DIAMOND

Msanii nguli katika kuiga sauti za
watu maarufu MC Babu Ayoub
aliyewahi kutamba na wimbo wa
chaja ya kobe ameibuka na
kusema mkali wa ngololo
Diamond si mchawi.
Mkali huyu wa kibao cha chaja ya
kobe ambaye pia aliwahi
kushiriki katika wimbo wa ndiyo
mzee wa Prof.J alifunguka mbele
ya mwandishi wetu. ALisema
“Diamond si mchawi ila
anajithamini kama msanii,anajua
umuhimu wake anajitambua na
hata kama hajitambui basi
anawashauri wazuri kwa maana
ya menejiment.anajituma kwani
anajua kucheza na muda na yuko
kibiashara zaidi si kama wasanii
wengine waliowahi kuhit,jamaa
najua pia kucheza na
media ,ukimpa nafasi hafanyi
makosa.Aidha msanii huyu
anayetegemea kuja na kibao
chake kipya amedai msanii
Diamond ana haki ya kuwa hapo
alipo lakini pia itakuwa ni
fundisho kwa wasanii wengine
waliohiti na watakaohit.

BABY MADAHA APIGWA CHINI NA RECORD LABEL YAKE YA CANDY AND CANDY YA UKO KENYA NA KUPOKONYWA GARI, KISA NI UMALAYA

Mwanamuziki na muigizaji baby
Joseph madaha amefunguka na
kusema kuwa kweli ameamini
uchawi na kupigana juju vipo
kwenye gemu kwani mambo
yaliyomtokea hivi karibuni
haelewi hata imekauje.
Chanzo nini?
Hapo siku za nyuma baby
Madaha alipatikana na dhahama
ya kukumbwa na kashfa nzito
sana ya kujiuza kwa dau la
milioni kumi kwa jamaa mmoja
hivi mitaa ya Dar es Salaam
Jambo lilolopelekea yeye kupigwa
chini na Record label yake ya
Candy and Candy ya huko Kenya
na kupokonywa gari aina ya AUDI
TT aliyokuwa akitembelea huku
akiharibu pia uhusiano wake na
bosi wa record label hiyo – Joe
kairuki ambaye pia anadaiwa
kuwa mpenzi wake.
Je ni Kweli alijiuza?
Baby Madaha ambaye amerudi
nchini hivi karibuni tokea Nairobi
alipoenda “ku-solve” ishu yake
hiyo na label hiyo anasema yani
hata haelewi kitu gani kilitokea
siku hiyo ingawa mpaka
akaandikwa kama alienda kujiuza,
anachokumbuka ni kupigiwa simu
na mtu asiyemfahamu an
kumwambia anataka wafanye
naye kazi ya kusambaza filamu
yake mpya ya Gal Bladder
ambaye inatikisa soko kwa sasa.
Baada ya kufika hapo waliongea
vizuri na kuondoka ghafla kabla
ya kuja kusoma kesho yake kuwa
alikuwa anajiuza kitu ambacho
ansema hajui kimetoka wapi.
“Yani hata sielewi ilikuaje
nikaenda kukutana na yule jamaa,
ilikuwa ni kama muujiza hivi,
mwanzo nilisita sana ila
nikashangaa nimefika tu pale bila
kujielewa, ni vitu vya ajabu sana”
alieleza baby Madaha.
Uhusiano wake na Label hiyo
ukoje sasa?
Akizungumza na bongomovies,
baby amesema kwa sasa kila kitu
kipo sawa kwani alipoenda Kenya
waliongea vizuri na bosi wake
huyo na kumaliza tofauti zao na
sasa amerudi nchini kusambaza
filamu yake hiyo mpya ya Gal
bladder huku akijiindaa kupiga
show kwenye tour yake
aliyoiandaa jina la Top Up and
Refill itakayofanyika mwezi ujao
wa tatu.
Mwenyewe anasemaje zaidi?
Hata wafanyaje, waniroge,
wanichafue, i’m a bad gal, na
sibabaishi na vijimaneno vya
watu hata kidogo, sitoki candy
and Candy hata waloge kwa
waganga wote duniani. Kama
walifikiri nimeumbuka, wajue
watasubiri sana. Nikitoka kenya
naenda Holywood tu!