NI kweli ukistaajabu ya Musa
utayaona ya Firauni! Fumanizi la
aina yake lilitokea juzikati
asubuhi ya saa 2, Mtaa wa
Mbwela, Tandika jijini Dar
ambapo mjamzito aliyejulikana
kwa jina la Semeni alipata
‘kichaa’ cha muda baada ya
kumfumania mumewe, Dullah
akiwa na mwanamke mwingine
chumbani kwao, Risasi Jumamosi
lina kisa kizima.Akisimulia mkasa
huo, Semeni mwenye ujauzito wa
miezi 6 alisema kabla ya tukio
aligombana na mumewe akarudi
kwao kwa muda wa siku mbili
lakini walikuwa wakiwasiliana
mpaka asubuhi ya tukio ambapo
alimpigia simu kumwambia
anafuata nguo kwa vile
anakwenda kliniki.
“Nilipokuwa njiani nilimpigia simu
mume wangu, nikamwambia
nimekaribia, lakini akasema yeye
amekwenda Posta.
“Pamoja na majibu hayo,
niliamua kwenda. Nilipofika
nilikuta mlango umefungwa kwa
ndani, nikampigia simu mume
wangu, akasisitiza hakuna mtu,
yeye yupo Posta.
“Nilichungulia na kuona funguo,
nikajua kuna mtu ila hataki
kunifungulia, hapo wasiwasi
ukazidi kwamba huenda kuna
jambo linaloendelea,” alisema
Semeni.
Mwanamke huyo aliendelea
kuanika kwamba kufuatia hali
hiyo aliwaita majirani ambao
ilibidi wamtishe mtu aliye ndani
kwamba asipofungua watavunja
mlango, ndipo mlango
ukafunguliwa na kumkuta Dullah
akiwa na mwanamke mwingine
chumbani, lakini mumewe huyo
alichoropoka na kukimbia.
“Nilishtuka, nikapiga kelele ya
mshangao kutokana na kitendo
alichokifanya mume wangu,
kumleta hawara mpaka kwenye
chumba tunacholala!
“Sijaamini kilichotokea! Yule ni
mume wangu, amewezaje
kumleta mwanamke ndani ya
chumba tunacholala tena kuna
wapangaji wenzangu
wameshuhudia,” alisema
mwanamke huyo huku akilia
machozi.
Akaendelea: “Mimi hapa
nyumbani siachiwi hela ya kula,
kila siku nakula nyumbani kwetu,
nikijua labda mume wangu hana,
kumbe anamalizia kwa hawara!
Jamani inaniuma sana, kama
hivyo bora amuoe basi tuje tuishi
wote au aniache akae yeye.”
Akizungumza na gazeti hili kwa
uso ‘uliochunwa’, mwanamke
aliyedaiwa kufumaniwa,
Mwanaidi huku akiwa
‘ametaitiwa’ ndani, alijitetea
kuwa hakufahamu kama Dulla
ana mke.
“Mimi aliniambia hana mke wala
mtoto na ndiyo maana nilikubali
kuanzisha uhusiano wa kimapenzi
na yeye si vinginevyo, kama
ningejua nisingekubali kuja, kwa
hiyo siyo kosa langu,” alisema
Mwanaidi.
Baada ya hali kutulia, baba mzazi
wa Dullah ambaye anaishi jirani
aliitwa kuamua ugomvi huo na
kuamuru wote waende nyumbani
kwake ambapo aliagizia gari.
Wawili hao walipofika nyumbani
kwa mzazi huyo walimshusha
Semeni na kumtaka atangulie
ndani, alipoingia tu, nyuma
dereva alitakiwa kuondoka gari
hilo kwa kasi huku Mwanaidi
akiwemo ndani ili kumnusuru.
Baada ya kubaini ‘triki’ hiyo,
Semeni alijirusha chini kwa
hasira na kujigalagaza kisha
kulikimbiza gari hilo bila
mafanikio.
0 comments:
Post a Comment