ads

Saturday, March 1, 2014

MASKINI AFANDE SELE...INASIKITISHA SANA...SOMA ZAIDI HAPA...!!!

SIKU chache baada ya kuzagaa
kwa taarifa za kuachana na
mkewe mama Tunda, mfalme
wa Rhymes, Seleman Msindi
‘Afande Sele’ ameibuka na
kusimulia mambo ya
kusikitisha waliyopita katika
safari ya maisha yao.
Akizungumza na wanahabari
wetu ndani ya Ukumbi wa
Meeda, Sinza-Mori, Dar, juzi
Afande alisema hadi kufikia
hatua ya yeye kutangaza kuwa
ameachana na mama Tunda
ambaye amedumu naye kama
mume na mke kwa zaidi ya
miaka 10, alikuwa akivumilia
mambo mengi na mwisho
kuamua kuachia ngazi.
Afande Sele akiwa na familia
yake.
“Nilikuwa nikielezwa mengi
kuhusu mke wangu,
nilishapigiwa simu na
kuambiwa mke wangu
anagombaniwa na wanaume
usiku klabu lakini huwa mimi
siyo mtu wa kuishi kwa hisia,
nilivumilia nikiamini
atajirekebisha, haikuwa hivyo.
“Japo sikuwa na uthibitisho wa
moja kwa moja, lakini
nyumbani alikuwa siyo mtu
wa kutulia, amekuwa
akinizunguka hadi kwa
washkaji zangu wa karibu.
Kuna jamaa alichoshwa na
habari hizo akanifuata na
kuniambia hata kama lakini
uvumilivu wangu ulizidi,”
alisema Afande kwa hisia.
Akiendelea kushusha
masikitiko yake mbele ya
kinasa sauti cha Risasi
Jumamosi, Afande alienda
mbele zaidi kwa kusema mbali
na mkewe huyo kumsaliti kwa
wanaume tofauti wakiwema
marafiki zake, ilifika wakati
mama Tunda akawa
anachukua fedha ndani na
kwenda kutumia na wanaume.
Alisema alitumia mwanya wa
mkali huyo wa mashairi
anapokuwa amesafiri katika
shoo mbalimbali na kuachiwa
fedha za matumizi pamoja na
ujenzi wa nyumba yao mpya,
kutanulia.
“We acha tu, yaani fedha za
matumizi, ujenzi nilikuwa
namuachia lakini cha
kusikitisha ni kwamba
alizitumia kutanulia, jambo
ambalo nililizidi kunitia
umaskini na machungu
ukizingatia jamii inaniheshimu
kama msanii, mbaya zaidi
wananchi wamenitaka
nigombee ubunge Morogoro
Mjini,” alisema Afande.
Akizidi kushusha ‘vesi’, Afande
alitiririka kuwa kuna wakati
aliwahi kupewa taarifa na
rafiki yake mwingine aishie
Kurasini jijini Dar ambaye
alilamika juu ya mkewe kufika
kwa jamaa huyo na kuazima
fedha bila kuzilipa.
Kwenye aya nyingine, mkali
huyo alisema anakumbuka
jinsi alivyoishi na familia yake,
mkewe, wanaye Tunda na
Ahsante Sanaa lakini hana jinsi
kwani ameona bora kuachana
kwani umri wake una mruhusu
kuoa mke mwingine siku
ikitokea.
“Nakumbuka maisha kidogo ya
furaha na familia, mama
Tunda atabaki kuwa mama wa
watoto wangu lakini kamwe
hawezi kurudi kwangu kwani
itakuwa ni aibu juu ya aibu,”
alisema.
Afande aliachana na mama
Tunda mwishoni mwa mwaka
jana alipotimba jijini Dar
katika shughuli zake za kikazi
na kumuachia mkewe fedha za
ujenzi lakini aliporejea
nyumbani Morogoro, alikuta
mzazi mwenzake huyo
ameondoka nyumbani na
kuacha funguo, kila
alipompigia simu hakupokea.
Alipoulizwa kuhusiana na
shutuma zilizoporomoshwa na
Afande, mama Tunda
alitiririka:
“Alinipa Sh. milioni 3 za shoo
tu, tukanunua vifaa vya ujenzi
lakini siyo kwamba nilitanua
na wanaume, tena kama ni
kumfumania, mimi ndiye
nilimkuta na mwanamke
alitoka naye Fiesta Dodoma,
sikutaka tu kumsema, hizo
taarifa anazusha tu.
“Kwanza kuna mambo mengi
tu amenifanyia, alikuwa mlevi
kwani hadi wazazi wangu
walikuwa wakinishangaa sana,
sasa na mimi nikaona bora
niachane naye,” alisema mama
Tunda.

Whatsapp YAJA NA KASHESHE HIVI KARIBUNI LA KUWAUMBUA WAONGO

Kasheshe tena bonge la
kasheshe laja. Kwa kutumia
maspy wake wa kimataifa,
blog yenu mzigo imekuja na
taarifa ambayo italeta
usumbufu mkubwa katika
jamii ya watumia whatsapp
hapa Bongoland. Najua
mnajiuliza ni nini? Hata sisi
wakurugenzi, waandishi,
wafagizi wa hii blog ya
chekanakitime tuliduwaa
hivihivi kama wewe
ulivyoduwaa wakati tunasubiri
kuelezwa na spy wetu wa
kimataifa ni nini alichogundua
kuhusu watumiaji wa
Whatsapp.
Baada ya Whatsapp kuwa na
kale kamtindo kabaya ka
kuumbua watu kakusema 'Last
seen 2:00'na hivyo kuua kale
kakisingizio kuwa simu ilikuwa
imezima kwa kukosa chaji sasa
wanakuja na mpya zaidi. Kale
kakipengele katakuwa
kanataja hata ulipo, hivyo
katakuwa kakisomeka
mfano,'Last seen 2:00 Sokoni
Kariakoo'.
Sasa hii ni mbaya sana wakati
mtu kakutumia mesej...Baby
tumekusanyika hospitali
mamake rafiki yangu yu
mahututi' Huku Whatsapp
inakuonyesha 'Last seen 2:00
Coco Beach'... Kamtindo haka
kanategemea kuua mapenzi na
ndoa kadhaa ambazo mpaka
sasa zinaonekana kuwa imara
sana.

Friday, February 28, 2014

Download New Best song Anko Dunia ( Roshazy ft: Cress )

DOWN LOAD NEW BEST SONG DUNIA UTANDAWAZI by Yamala

https://www.hulkshare.com/yuskisskisiba/yamala[hulkplayer code="6gtmgsz03sao"]

MWANA DADA WEMA ATAJA SIFA ZA MWANAUME ANAYE MTAKA SOMA HAPA SIFAHIZO KAMA UNAZO

Mwanadada Wema Sepetu ambaye
pia aliwahi kuwa Miss Tanzania
2006 ambaye kwa sasa
anaendesha kampuni yake binafsi
iitwayo Endless Fame
inayojishughulisha zaidi na
utengenezaji wa Filamu
mbalimbali.
Kupitia kipindi cha Leo tena
February 28 Wema Sepetu
amekubali kutaja sifa za
mwanaume anayempenda kuwa na
mvuto kwake,swali lililoulizwa na
Watangazaji wa kipindi hicho ni
kuhusu mwanaume wa sifa gani
anayedhani anaweza kuolewa nae
ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio
shida je huyo mwanaume
nampenda,maana naweza kuja
kuchumbiwa lakini nisimpende”
“Mimi nampenda Mwanaume
mweusi,wanaume weupe sio
kwamba sijawahi kuwa nao lakini
nakuwa sina mzuka nao”.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake
na Diamond amekiri kwa
kusema’Kweli niko na Nasib -
Diamond na nadhani muda huu
kutakua na utulivu ndani yake,ule
utoto tuliokua tunafanya nadhani
ulikua utoto na imekua Power
Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo
tuna ni miaka 4 sasa,kwa sasa
tumeamua kuwa serious’.
Habari kwa Hisani ya Millard Ayo
Wema Sepetu pia kaandamana na
Ant Ezekiel kwenye interview ya
kipindi hicho kinachorushwa na
Clouds Fm.

Thursday, February 27, 2014

Polisi wa Uganda wamezuia kundi la wanawake waliopanga kuandamana kupinga sheria inayopiga marufuku picha chafu.

Polisi wa Uganda wamezuia
kundi la wanawake waliopanga
kuandamana kupinga sheria
inayopiga marufuku picha
chafu.
Chini ya sheria hiyo ni marufuku
kwa wanawake kuvalia mavazi
mafupi, yenye kubana mwilini
kiasi cha kuonekana mapaja na
makalio na sheti inayoonyesha
matiti.
Wanawake hao waliopanga
kuandamana mjini Kampala
walibeba mabano kupinga sheria
mpya baadhi wakuvalia mavazi
mafupi. Baadaye walikubaliwa
kukusanyika katika uwanja nje ya
ukumbi wa kitaifa.

Wednesday, February 26, 2014

DIAMOND ASEMA HAYA JUU YA WASANII WA WA TANZANIA KUHUSU MAJUNGU

Diamond Platnumz
kiukweli, nasikitishwa sana jins
baadhi ya wasanii kutwa
wanavyolazimisha kunitengenezea
ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na
sababu, mara wengine wakizusha
eti Nimewatusi kwenye Media,
Mara sjui Nimepost kuwakashif,
yaani ilimradi tu....kwanini
Wanamuziki wa Tanzania
Tunashindwa kubadilika... mbona
mi nahangaika na muziki wangu
kimpango wangu... Mnasema nyie
ndio mnaojua kuimba mie sijui
"sinatatizo"... Mnasema nyie ndio
wenye sauti nzuri yangu mbaya
"Sina tatizo"... sasa mbona tena
bado mnanifatilia na kutokujua
kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza
kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa
ya nchi yetu na kuleta heshima na
maendeleo nchini, kuliko kupika
majungu..... Watu wanataka kazi!

JE WAJUA MWANAMKE MWENYE ULIMI MREFU DUNIANI SOMA HAPA UPATE KUJUA

Pichani kushoto ni bi mdada
Chanel Tapper akionyesha urefu
wa ulimi wake
Chanel Tapper ni mwanafunzi wa
chuo cha California Marekani,
ndiye mwanamke wa kwanza
anayeshikilia rekodi ya dunia ya
kuwa na ulimi mrefu kupita
wanawake wote, inasemekana
anaulimi wenye urefu wa sentimita
9.7, baada ya kuingia katika kitabu
cha rekodi za dunia maarufu kama
Guiness , amesema anategemea
wahisani pamoja na hela
atakazopata ziweze kumuendeleza
katika kumaliza chuo na masomo
yake.

HOT PHOTOS...TANZANIAN ACTRESS LULU....!!YOU MUST SEE..

Tutumie picha zako ambazo ungependa kushare mitindo ya mavazi , swaggz na mapozi mautundu ya kinyamwezi
katika mtoko waleo leo

namba yakutuma ni
+255 (0) 655323305

BAADA YA MSANII PNC KUJITOA MTANASHATI NA KUMSINGIZIA UONGO USTAZ JUMA, ARUDI NA KUMPIGIA MAGOTI. CHEKI PICHA HAPA

Baada ya kutimuliwa
MTANASHATI msanii PNC arudi
mikono nyuma akimuomba boss
wake Ostaz Juma arudi tena
katika lebo hiyo. Picha hii
imeonekana katika account ya
facebook ya Ostaz Juma ikisema
“hahaha jamani mziki ni kazi
pnc arudi kuomba msamaha ili
aendelee kufanya kazi
mtanashati”
Na baadae mtu mzima Ostaz
akatupia video clip ikimuonyesha
PNC akiomba msamaha kwa
machungu kabisa hebu bonyez
CREDIT : DJ CHOKA

Tuesday, February 25, 2014

NISHA AMFANYIA SUPRISE MAMA YAKE HEMEDI PHD SOMA HAPA UJUE

Nisha amfanyia suprise mama
yake Hemedi PHD katika siku
ya kuzaliwa mama yake Hemedi
PHD ilikuwa kinondoni
barabarani akamwambia
hemedi kapata ajali alivyotoka
nje alikuwa kapagawa mara
waka mwimbia happy birth day
toyuuuuuuuuu...!!!
Ha ha haaa!!! Mama Hemedy
hoi tena kibaya zaidi siku hio
ilikuwa ndio siku ya
kumaliziwa Shooting ya Filamu
ya GUMZO ambayo kwa sasa
ipo mbioni kutoka,
Yani mama kutoka tu nje
akaona msongamano wa
magari watu kibao akaamini
kuwa mwanae kapata ajali
kweli kumbe ilikuwa ni katika
kumalizia kipande cha Filamu
ambapo Hemedi PHD
anatakiwa aonekane katika
ajali ya kugongwa na gari.. Du!
mama almanusura kuzimia.
Mama yake hemedi alifarijika
sana ilikuwa kipindi cha
shooting ya gumzo

Daktari FEKI akamatwa hospitali ya Muhimbili......Hili ni tukio la tatu kutokea

Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna  mbalimbali  Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza.Hospitali ya Muhimbili inawataka wafanyakazi wake wanaoshirikiana na madaktari vishoka kuacha tabia hiyo yenye athari kwa wagonjwa na taifa.Chama cha Madaktari nchini kimewataka wananchi kuwa  macho na madaktari wanaojitokeza kutaka kusaidia wagonjwa.Wakati daktari huyo akidai yeye ni daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifaza kiuchunguzi kuthibitisha kuwa ni feki.Hili ni tukio la tatu kutokea katika hospitali ya Muhimbili.

Monday, February 24, 2014

MWANA DADA MREMBO AFIA GEST JIJINI ARUSHA

MREMBO mmoja ambaye alihu-
dumu kwenye nyumba ya kulala
wageni na baa (jina tunalo)
iliyopo Tengeru, wilayani
Arumeru, mkoani Arusha,
Blandina Michael (33) amekutwa
amekufa kwenye moja ya vyumba
vya nyumba hiyo huku chanzo
cha tukio hilo kikihusishwa na
vitendo vya ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu
mmiliki wa nyumba ya wageni
moja ambaye pia anajihusisha na
biashara za madini (jina tunalo)
kwamba alimtoa kafara
mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa,
kila mwaka mtu mmoja katika
biashara zake hupoteza maisha
ghafla.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo
alipoongea na Uwazi juzikati
alikanusha vikali tuhuma hizo na
kueleza kuwa yeye ni muumini
mzuri wa imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana,
unajua kuna mwaka mwanaume
mmoja alikufa ghafla kwenye
nyumba yangu ya kulala wageni,
alikuja na mpenzi wake ila
alimeza Viagra ambazo hata
polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na
mimi tukio hilo wanaliunganisha
na hili kwamba nawatoa kafara,”
alisema.
Kifo cha Blandina kilitokea ndani
ya chumba huku mtu mmoja
anayedaiwa kuwa mpenzi wake
aliyejulikana kwa jina moja la
Timo, mkazi wa eneo hilo
akihojiwa na polisi.
Marehemu Blandina ambaye ni
mzaliwa wa mkoa wa Tanga,
anaelezwa na bosi wake huyo
kwamba alikuwa kama mtoto wa
familia yake kwa vile alimwamini
sana. Alifanya kazi hapo kwa
miaka 8 na hakuwa na tatilo la
kiafya.
Bosi huyo alisema mwili wa
marehemu uligundulika baada ya
mfanyakazi mwenzake wa kiume
kumpigia simu saa 2 asubuhi
ambapo simu yake ilikuwa ikiita
bila kupokelewa ndipo alipoamua
kwenda kumgongea katika
chumba hicho.
Alisema baada ya kufika
alishangaa kukuta mlango wa
chumba chake uko wazi na
alipochungulia alibaini kwamba
Blandina alikuwa amefariki dunia.
Hata hivyo, polisi baada ya kufika
na kuufanyia uchunguzi wa awali
mwili huo hawakugundua
kuwepo kwa jeraha lolote
linaloashiria kuuawa, ingawa
mwili huo ulipelekwa kufanyiwa
uchunguzi wa kitaalam katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru.

COVER YA FILAMU YA MPONZA DR.CHENI

Msanii wa filamu hapa nchini
anayefahamika kwa jina la Dr.
amejikuta katika wakati mgumu
baada ya bodi ya filamu Tanzania
kuzuia filamu yake mpya inayoitwa
'Nimekubali Kuolewa' kwa madai
ya cover iliyotumika katika kasha
la filamu hiyo inachochea ushoga.
Kufuatia madai hayo msanii huyo
amesema kuwa
bodi hiyo haikumtendea haki kwa
kuwa filamu yake ina lengo zuri la
kupinga ushoga na sio kuchochea.
Ameela bodi hiyo haikuangalia
maudhui na badala yake
imeangalia zaidi cover la filamu
hiyo
“Eti ushoga wangu uko kwenye
kujiremba sana, wamenionea,
lengo letu ni kukemea na kupinga
vikali vitendo vya ushoga na ndoa
za jinsia moja, huwezi kuelimisha
bila kuonesha madhara yake kwa
vitendo kama ilivyo kwenye filamu
hiyo. Amesema Dk Cheni.
Msanii huyu amekumbwa na hali
hiyo ikiwa ni muendelezo wa bodi
ya filamu kuzuia filamu ambazo
inazitilia mashaka.
Hata hivyo bodi hii imekuwa
ikilalamikiwa na baadhi ya wasanii
wakidai haitendi haki.

VIFO VYA WATOTO KUONGEZEKA KILA MWAKA KUTOKANA NA VITA VINAVYO ENDELEA DUNIA


Shirika la Misaada kwa watoto,
Save the Children, linasema
kuwa watoto milioni moja
hufariki dunia kila mwaka
katika siku yao ya kwanza ya
maisha.
Katika ripoti mpya ya shirika hilo
la misaada kwa watoto linasema
vifo vya watoto wachanga
vimesalia kuwa moja ya aibu za
dunia ya sasa.
Hali ya watoto ni mbaya zaidi
hasa katika mataifa
yanayokabiliwa na mizozo.
Mwandishi wa BBC aliye Sudan
Kusini, Anne Soy, amesema kuwa
katika mazingira ya sasa ya Sudan
Kusini, watoto na wanawake, hasa
wale waja
wazito wanaokabiliwa na athari
nyingi za vita vinavyoendelea
nchini humo.
Amesema kuwa kutokana na vita
watoto, walioandamana na wazazi
wengine wakiwa pekee,
wanaungana na akina mama
kutembelea mwendo
mrefu ili kujiepusha na vita vya
kikabila vinavyoendelea nchini.
Miundo msingi katika Sudan
Kusini, kama vile hospitali ni
chache sana jambo ambalo
linatatiza maisha ya wanawake na
watoto.
Katika hospitali ya mji wa Nimule
kwenye mpaka wa Sudan Kusini
na Uganda Kuna vitanda 174
pekee hospitalini idadi ambayo
haiafikiana kamwe
na maelfu ya wagonjwa na
wahasiriwa wa vita .
Save the children inasema kuwa
vita vinawaathiri zaidi watoto
huko Syria, Jamhuri ya Afrika ya
Kati CAR na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Shirika la Save the Children
linasema kuwa vifo hivi vingi
vinaweza kuzuiliwa.

VIJIMAMBO KATIKA JAMII NIPE NIKUPE SAMAKI NA NGONO KENYA

Inakadiriwa takriban watu milioni
moja na nusu wanaishi na virusi
vya HIV na maradhi ya UKIMWI
nchini Kenya.
Wavuvi vijijini huwapa wauza
samaki wanawake samaki kama
malipo kwa kufanya nao ngono
badala ya pesa.
Lakini sasa mashirika ya misaada
yanajaribu kubadilisha tabia hii,
ijulikanayo kama 'kubadilisha
ngono na samaki'.
Wanawahimiza wanawake
wanunue mashua zao wenyewe.
Mariam Omar ana zaidi toka
magharibi mwa Kenya.

PICHA ZA SHOW NZIMA ALIYOIFANYA DIAMOND NA WCB KWENYE COCA COLA PARTY-COCO BEACH

show hii ilikuwa ni bab kubwa kwa msanii huyu Diamond alionekana kulitawala jukwaa vyema kwa muda mrefu na kupelekea mashabiki wa kufurahia onesho hilo kuliko msonesho mengine hapa Dar

Download New Best song 2014 Roshazy ft. Creas

MTANZANIA SABRINA ABAKWA NA WANIGERIA WATANO CHINA, APOTEZA MAISHA

Mwandishi Wetu
AMA kweli dunia hadaa,
ulimwengu shujaa! Kumeibuka
mchezo mchafu,
kuna Watanzania wanawachukua
warembo nchini na kuwapeleka
China kwa ahadi kwamba
wanakwenda kufanya kazi saluni,
wakifika kule wanawanyang’anya
paspoti na kuwauza kwa
wanaume (ukahaba), sasa
yamemkuta Mbongo aitwaye
Sabrina au Habiba, Ijumaa
Wikienda lina mkasa wa
kusikitisha.
Habari za uhakika kutoka kwa
chanzo chetu nchini humo
zilisema kuwa, Sabrina (24),
alifariki dunia Alhamisi iliyopita
kufuatia kubakwa na wanaume
watano, raia wa Nigeria ambao
wamo nchini humo kibiashara.
Tukio hilo lilijiri kwenye hoteli
moja iliyopo kwenye Mji wa
Guangzhou ambao umejaa
wageni wengi, wakiwemo
Watanzania.
SIKU YA TUKIO
Rafiki wa karibu wa Sabrina,
Saada alisema siku ya tukio,
marehemu akiwa katika harakati
zake za kutafuta wateja alikutana
na Mnigeria mmoja ambaye
walipatana kulala wote kwa usiku
mzima.
“Kumbe yule Mnaigeria alikuwa
na wenzake wanne. Usiku
walimwingilia wote kwa nguvu
kwa kumbaka mpaka akapoteza
maisha palepale. Ni ukatili
mkubwa.
“Wale watu walipogundua
Sabrina amekufa waliuchukua
mwili wake na kuutupa chini
kutoka ghorofa ya tano,” alisema
rafiki huyo.
MAITI YAKUTWA HAINA FIGO,
MOYO
Habari zaidi zilidai kuwa mpaka
juzi (Jumamosi) madaktari
waliokuwa wakiuchunguza mwili
wa Sabrina waligundua hauna
figo na moyo, jambo linalozidi
kuzua hofu juu ya muaji yake.
NI BIASHARA ILIYOIBUKA CHINA?
Ilidaiwa kuwa nchini China
imeibuka biashara ya viungo
mbalimbali vya binadamu
ambapo ili vipatikane ni lazima
mwenye viungo hivyo auawe kwa
njia yoyote.
SABRINA AFA, MGANDA APOTEA
Mtoa habari wetu alisema wakati
Wabongo wakiwa kwenye
maombolezo ya kifo cha
Mtanzania huyo, mrembo
mwingine raia wa Uganda, nchi
ambayo imo ndani ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki amepotea katika
mazingira ya kutatanisha nchini
humo.
Baadhi ya watu wana wasiwasi
kuwa kupotea kwa msichana
huyo kunahusiana na kushamiri
kwa biashara ya viungo vya
binadamu.
SABRINA ALIKWENDAJE CHINA?
Mwezi Julai, mwaka jana, Sabrina
alikwenda nchini humo
akidanganywa na mwanamke
mmoja kwamba atapata kazi
kwenye saluni ya wanawake lakini
baada ya kufika alijikuta
akiingizwa kwenye biashara ya
ukahaba bila ridhaa yake mpaka
alipokutwa na mkasa huo
uliopoteza maisha yake.
TAHADHARI KWA WAREMBO
WANAOKWENDA CHINA KUFANYA
KAZI SALUNI
Imebainika kuwa, kumeibuka
wimbi la Wabongo wanaofanya
‘uwakala’ wa kuwachukua
wasichana wa Kitanzania kwa
kuwadanganya kwamba
wanakwenda kufanya kazi za
saluni nchini humo.
Mara baada ya kufika, wasichana
hao hunyang’anywa paspoti ili
washindwe kuondoka nchini
humo na kushinikizwa kujiuza
(ukahaba) huku waliowapeleka
wakipokea fedha kutoka kwa
wateja.
KUIKOMBOA PASPOTI
Habari zilisema kuwa mhusika
hurejeshewa paspoti yake baada
ya malipo yake kwa ‘wakala’
kufikia dola za Marekani 8,000
(kama shilingi milioni 12), ndipo
huachiwa ‘huru’ kuendelea na
maisha yake.
Wengi wakishaachiwa hushindwa
kurejea Bongo na kujikuta
wakiendelea kuuza miili katika
mahoteli na klabu huku
wakikutana na majanga
mbalimbali.
MASOGANGE, KAJALA NA DIDA
Watanzania waishio nchini humo
wamewatahadharisha mastaa wa
Bongo, wakiwemo Mtangazaji wa
Radio TimesFM, Khadija Shaibu
‘Dida’, msanii wa filamu Kajala
Masanja na Video Queen Agnes
Gerald ‘Masogange’ ambao
hupenda kwenda nchini humo
kwa shughuli zao, kutokubali
kuwa karibu na mawakala wa
kuchukua wasichana Bongo kwa
kuwadanganyia kazi ya saluni
kwani wanaweza kujikuta pabaya
siku moja.
DIDA
Ijumaa Wikienda lilimsaka Dida
siku ya Jumamosi iliyopita na
kumuuliza kuhusu kuwepo kwa
mawakala hao ambapo alikiri
kusikia huku akisema warembo
wenyewe wanapaswa kuwa
macho na udanganyifu huo.
“Najua wapo Wabongo
wanaofanya shughuli hiyo, si
China tu hata India, unapelekwa
kwa ahadi ya kazi ya saluni,
ukifika hamna cha saluni wala
nini? Warembo wawe makini
jamani, nenda China kama una
uwezo wako mwenyewe kufanya
‘shoping’ lakini si kupelekwa,”
alisema Dida.
BALOZI WA TANZANIA-CHINA
Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta
Balozi wa Tanzania nchini China,
Luteni Jenerali Mstaafu
Abdulrahman Shimbo ili
azungumze lolote kuhusu tukio la
Sabrina, lakini simu yake
ilionekana kutokuwa hewani kwa
muda mrefu.

Sunday, February 23, 2014

HUU NDIO UJIO MPYA WA MDADA RAY C...!!!SOMA ZAIDI HAPA...

Anaitwa Rehema Chalamila kwenye stage ya muziki tunamjua kama Ray C. Kitu kikubwa kinachosubiriwa kutoka kwake hivi sasa kazi zake mpya kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. Kitu cha kusubiria sio hicho tu bali Ray C Foundation ni kitu kingine kitakacho kuja kutoka kwa Ray C. Ameshare ujio wa foundation hii kwenye ukurasa
wake wa instagram na
kudokeza kwa maneno
“Coming soon stay tuned!!!!!”
japokuwa hakuweka wazi kazi
ambayo itafanywa na
foundation hiyo.