ads

Saturday, March 8, 2014

PICHA ZA DULLY PAMOJA NA MISS MOROGORO ZINAZOLETA UTATA HIZI HAPA.

Thursday, March 6, 2014

Picha 6 za Nicki Minaj zinazoangaliwa sana hivi sasa kwenye mtandao...!

Unaambiwa Nicki Minaj anajipanga kuja na muonekano mpya pamoja akijiandaa na kutoka na album au mixtape.Mara nyingi picha zinazotoka kwenye media zinazomuonyesha Nicki Minaj akiwa na muonekano wa Barbie kama kawaida yake. 

Lakini hizi picha alizozitoa mwenyewe ameonekana kuwa na nywele zake mwenyewe bila vitu vingine anavyojitupiaga.


HATARII..MFUNGWA AMBAKA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI HUKO GEITA...!!!


MFUNGWA aliyekuwa
akitumikia kifungo cha miezi
sita katika Gereza la Butundwe
wilayani Geita amembaka
mwanafunzi wa Shule ya
Msingi Luhuha iliyoko Tarafa
ya Butundwe na kumuumiza
sehemu zake za siri, shingoni
na kwenye jicho la kulia.
Mwanafunzi huyo mwenye
umri wa miaka 15 (jina
linahifadhiwa) alitendewa
unyama huo na mfungwa
aliyejulikana kwa jina la
Godfrey Seleman (19) Februari
26, mwaka huu majira ya saa
9:00 alasiri wakati
mwanafunzi huyo alipokuwa
akichanja kuni na wanafunzi
wenzake.
Akieleza jinsi alivyofanyiwa
unyama huo, mwanafunzi
huyo alisema alipotoka shuleni
akiwa na wasichana wenzake
watano walikwenda kuchanja
kuni ndipo walipomuona
mfungwa huyo akiwa amevaa
sare, lakini baadaye alitoweka
ghafla na kurudi akiwa
amejipaka masizi usoni, akiwa
uchi kisha kuanza kumfukuza
yeye huku wenzake wengine
wakifanikiwa kukimbia huku
wakipiga kelele.
Alisema alizidiwa mbio na
mfungwa huyo ambapo
alimshika kisha kumkaba
shingoni na kumwangusha
chini na kuanza kumtendea
unyama na kumsababishia
maumivu makali sehemu zake
za siri.
“Baada ya kutendewa unyama
huo nilitoka eneo hilo ambapo
njiani nikutana na mama
mmoja nikamwelezea mkasa
ulionipata alinionea huruma
ambapo alinipeleka ofisi ya
kijiji ambako niliandikiwa
barua kuwahi polisi,
nikapelekwa hospitali ambako
walinifanyia vipimo,” alisema
binti huyo.
Aliendelea kusema kuwa
mfungwa huyo alimpiga na
kumuumiza katika jicho lake la
kulia ambalo limevimba na
kuwa bado anasikia maumivu
makali jichoni na
shingoni.Kamanda wa polisi
mkoani hapa amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo
ameliita la kinyama
lisilopaswa kutendwa na mtu
mwenye akili timamu.Alisema
mfungwa huyo mweye na
namba 244/2013 alikuwa atoke
kifungoni mwezi ujao, tayari
ametiwa mbaroni na
atafikishwa mahakamani
upelelezi utakapokamilika