ads

Monday, February 17, 2014

WASTARA JUMA APATA AJALI MBAYA YA GARI

1:15 AM By Unknown , No comments

MAJANGA! Siku chache baada ya
hivi karibuni kudaiwa kunywa
sumu, staa mkubwa wa sinema
Bongo, Wastara Juma amepata
tena ajali mbaya.Habari za
uhakika zilizolifikia gazeti namba
wani la burudani Bongo, Ijumaa
Wikienda mwishoni mwa wiki
iliyopita zilieleza kuwa siku ya
tukio Wastara alitoka nyumbani
kwake Tabata-Bima, Dar na gari
lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili
ya kwenda kununua umeme.
Akizungumzia tukio hilo kwa
masikitiko, Wastara aliliambia
gazeti hili kuwa kabla ya kufika
kwenye kituo cha kununulia
umeme (Luku) alikutana na lori
kubwa lililokuwa kwenye mwendo
kasi huku likiwa limewasha taa
fulu.
Alisema kuwa alijaribu kulikwepa
lakini lilimsukuma na kujikuta
akiingia mtaroni kutokana na
barabara kuwa nyembamba
ambapo aliumia sehemu za
kichwani na mguuni kwa ndani.
Wastara alisema baada ya hapo
alikimbizwa katika Hospitali ya
TMJ, Dar ambapo alisafishwa
majeraha (dressing) kisha
akapatiwa matibabu na baadaye
aliruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nimenusurika kifo, namshukuru
sana Mungu kwani ajali ilikuwa
mbaya nilihamishwa kwenye siti
niliyokuwa nimekaa na kurushwa
kwenye siti nyingine huku
nikijigonga na kuumia kichwani.
“Pia gari langu limeharibika sana,
kioo chote kimevunjika, sielewi
kwa nini haya yote yananitokea.
“Namuomba Mungu anisaidie
maana naona mambo
yanakwenda ndivyo sivyo na kwa
nguvu zangu mwenyewe
siwezi,”alisema Wastara.
Hata hivyo, Wastara kwa sasa
anaendelea vizuri japokuwa bado
anaumwa kichwa na mguu.
Wastara ameshapata ajali mara
kadhaa ikiwemo ile ya pikipiki
aliyopata mwaka 2008 akiwa na
aliyekuwa mumewe, Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi
akatwe mguu wa kulia. Pia
aliwahi kupata nyingine ya gari
akiwa na Sajuki.
Kwa mujibu wa watu wa karibu
wa Wastara, kuna watu
wanamtakia mabaya ili amfuate
Sajuki aliyefariki Januari 2, mwaka
jana.

0 comments:

Post a Comment