Serikali ya Nigeria imekiri makosa ambayo yalisababisha mkanyagano wa watu pale walipokuwa wakihudhuria zoezi la serikali la kuwaajiri watu kazi katika miji kadhaa Nchini Nigeria.Maelfu ya watu waliokuwa na hamu kubwa ya kupata ajira, walijitokeza kwa wingi katika zoezi la mitihani ya kutafuta kazi kote Nchini humo.Walikuwa wamejitokeza katika ofisi za wizara ya uhamiaji.Watu saba waliuawa katika uwanja wa taifa mjini Abuja.Waziri wa mambo ya ndani Abba Moro, aliambia CSW kuwa utaratibu ulikosekana katika uwanja huo kiasi cha kusababisha vurumai hilo.Zaidi ya thuluthi moja ya watu walio chini ya umri wa miaka 25 hawana ajira nchini Nigeria.
0 comments:
Post a Comment