ads

Sunday, March 16, 2014

MASKINI MTOTOANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE KISA....

7:55 AM By Unknown , , No comments

Mtukioyakikatili yameendelea kushika kasi wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mtoto aitwayeSaid Siraji/SaidJoshuaamelazwa katika Hospitali ya wilaya usiku wa kuamkia leo, baada ya kunusurika kifo katika jaribio la kuchinjwa nababayake mzazi aliyejulikana kwa jina laSalvatory.Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya-Kahama; DaktaJosephFwoma amesema Siraji amefikishwa hospitalini hapo leo alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia huko akivuja damu shingoni.Dakta Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.Kwa mujibu wamamamzazi wa Mariamu Idd(35) amesema, Mtoto Siraji jana alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwisha achana siku nyingi.Mariam amesema, awali Salvatory alikuwaakimchukua Sirajimarakwa mara na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye kumrudisha akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya.Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha tukio hilo inasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa akili.

0 comments:

Post a Comment