SIKU chache baada ya kuzagaa
kwa taarifa za kuachana na
mkewe mama Tunda, mfalme
wa Rhymes, Seleman Msindi
‘Afande Sele’ ameibuka na
kusimulia mambo ya
kusikitisha waliyopita katika
safari ya maisha yao.
Akizungumza na wanahabari
wetu ndani ya Ukumbi wa
Meeda, Sinza-Mori, Dar, juzi
Afande alisema hadi kufikia
hatua ya yeye kutangaza kuwa
ameachana na mama Tunda
ambaye amedumu naye kama
mume na mke kwa zaidi ya
miaka 10, alikuwa akivumilia
mambo mengi na mwisho
kuamua kuachia ngazi.
Afande Sele akiwa na familia
yake.
“Nilikuwa nikielezwa mengi
kuhusu mke wangu,
nilishapigiwa simu na
kuambiwa mke wangu
anagombaniwa na wanaume
usiku klabu lakini huwa mimi
siyo mtu wa kuishi kwa hisia,
nilivumilia nikiamini
atajirekebisha, haikuwa hivyo.
“Japo sikuwa na uthibitisho wa
moja kwa moja, lakini
nyumbani alikuwa siyo mtu
wa kutulia, amekuwa
akinizunguka hadi kwa
washkaji zangu wa karibu.
Kuna jamaa alichoshwa na
habari hizo akanifuata na
kuniambia hata kama lakini
uvumilivu wangu ulizidi,”
alisema Afande kwa hisia.
Akiendelea kushusha
masikitiko yake mbele ya
kinasa sauti cha Risasi
Jumamosi, Afande alienda
mbele zaidi kwa kusema mbali
na mkewe huyo kumsaliti kwa
wanaume tofauti wakiwema
marafiki zake, ilifika wakati
mama Tunda akawa
anachukua fedha ndani na
kwenda kutumia na wanaume.
Alisema alitumia mwanya wa
mkali huyo wa mashairi
anapokuwa amesafiri katika
shoo mbalimbali na kuachiwa
fedha za matumizi pamoja na
ujenzi wa nyumba yao mpya,
kutanulia.
“We acha tu, yaani fedha za
matumizi, ujenzi nilikuwa
namuachia lakini cha
kusikitisha ni kwamba
alizitumia kutanulia, jambo
ambalo nililizidi kunitia
umaskini na machungu
ukizingatia jamii inaniheshimu
kama msanii, mbaya zaidi
wananchi wamenitaka
nigombee ubunge Morogoro
Mjini,” alisema Afande.
Akizidi kushusha ‘vesi’, Afande
alitiririka kuwa kuna wakati
aliwahi kupewa taarifa na
rafiki yake mwingine aishie
Kurasini jijini Dar ambaye
alilamika juu ya mkewe kufika
kwa jamaa huyo na kuazima
fedha bila kuzilipa.
Kwenye aya nyingine, mkali
huyo alisema anakumbuka
jinsi alivyoishi na familia yake,
mkewe, wanaye Tunda na
Ahsante Sanaa lakini hana jinsi
kwani ameona bora kuachana
kwani umri wake una mruhusu
kuoa mke mwingine siku
ikitokea.
“Nakumbuka maisha kidogo ya
furaha na familia, mama
Tunda atabaki kuwa mama wa
watoto wangu lakini kamwe
hawezi kurudi kwangu kwani
itakuwa ni aibu juu ya aibu,”
alisema.
Afande aliachana na mama
Tunda mwishoni mwa mwaka
jana alipotimba jijini Dar
katika shughuli zake za kikazi
na kumuachia mkewe fedha za
ujenzi lakini aliporejea
nyumbani Morogoro, alikuta
mzazi mwenzake huyo
ameondoka nyumbani na
kuacha funguo, kila
alipompigia simu hakupokea.
Alipoulizwa kuhusiana na
shutuma zilizoporomoshwa na
Afande, mama Tunda
alitiririka:
“Alinipa Sh. milioni 3 za shoo
tu, tukanunua vifaa vya ujenzi
lakini siyo kwamba nilitanua
na wanaume, tena kama ni
kumfumania, mimi ndiye
nilimkuta na mwanamke
alitoka naye Fiesta Dodoma,
sikutaka tu kumsema, hizo
taarifa anazusha tu.
“Kwanza kuna mambo mengi
tu amenifanyia, alikuwa mlevi
kwani hadi wazazi wangu
walikuwa wakinishangaa sana,
sasa na mimi nikaona bora
niachane naye,” alisema mama
Tunda.
0 comments:
Post a Comment