KOCHA wa Manchester
United, David Moyes
amesema usajili wa Juan
Mata na kurejea kwa Robin
van Persie na Wayne Rooney
kumerudisha morali Old
Trafford.
Van Persie amerejea uwanjani
baada ya kukosa mechi 11
kutokana na kuwa majeruhi
na kufunga katika ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Cardiff,
huku Mata akifanya kazi nzuri
baada ya kusajiliwa kwenye
dirisha dogo kwa pauni
milioni 37.1 akitokea Chelsea.
"Morali yangu imerudi, kwa
sababu najua kwamba
wachezaji wazuri wamerudi,"
alisema Moyes.
"Lakini bado nataka kushinda
na kucheza vizuri zaidi kwa
hiyo usidhani kwa sababu
nimeshinda leo (juzi) ndio
sababu ya kufurahi".
"Nina furaha kwa pointi tatu
nilizopata lakini wapi, nataka
kwenda na malengo ya wapi
nataka timu yangu icheze,
bado nahisi nina kazi kubwa
ya kufanya".
Ushindi huo umeifanya
Manchester United izidishe
ushindani katika kuwania
nafasi ya nne dhidi ya Everton
na Tottenham, lakini bado
wana tofauti ya pointi sita
dhidi ya timu inayoshika
nafasi ya nne Liverpool baada
ya kikosi hicho cha Brendan
Rodgers kuifunga Everton.
Na Moyes alikiri kwamba ujio
wa Mata, ambaye alicheza
vizuri licha ya kufanyiwa
mabadiliko kunampa namna
ya kupanga timu yake.
Katika mechi dhidi ya Van
Persie alifunga bao la kwanza
kabla Ashley Young hajafunga
bao la pili na la ushindi.
United imepoteza mechi nne
kati ya sita za mwisho
ikifanya vibaya kwenye Ligi na
kwenye makombe mbalimbali.
"Juan alifanya vizuri sana
ametengeneza nafasi nzuri
sana katika dakika 30 za
mwanzo," aliongeza Moyes.
"Tutamtumia na yeye
atatutumia, nilitaka kuwaona
yeye na Robin pamoja usiku
huu (juzi)," alisema.
0 comments:
Post a Comment