Msanii wa HipHop kutoka
Tanzania, Ambwene Yesaya
amekanusha uvumi uliokuwa
umezagaa nchini Kenya wa
kumuandikia baadhi ya nyimbo
mkali wa Kioo kutoka Kenya,
Jaguar.
Katika mahojiano aliyofanyiwa
nchini Kenya alikokuwa ameenda
hivi karibuni, AY amesema hajawai
kumuandikia wimbo wowote
Jaguar na hata wimbo wao
‘Nimetoka Mbali’ kila mtu aliandika
mashairi yake.
“Jaguar ni mmoja wa marafiki
zangu. Tumefanya kazi pamoja na
hakuna ukweli wowote kuhusiana
na tetesi za mimi kumuandikia
mashairi ukizingatia amekuwepo
kwa muda mrefu kwenye gemu ya
muziki hivyo kumfanya kuwa
miongoni mwa wasanii wenye
uzoefu wa kutosha na kufanya
vizuri hata ukitazama ngoma
niliyowahi kufanya nae ya
Nimetoka Mbali, kila mmoja wetu
aliandika mashairi yake kivyake
hivyo huna haja ya kubisha kwa
uwezo mkubwa alionao na naamini
ni ushahidi tosha,” alisema.
Pia AY amepinga muziki wake
kuathiriwa na Diamond kwakuwa
kila mtu ana malengo yake katika
muziki wake.
“Kila msanii ana mipango na
mikakati yake ya kufikia malengo
aliyojiwekea, sipo kujilinganisha na
mtu yoyote, ushindani wangu ni
kwa yule anayetaka kujaribu
kutengeneza mkwanja mkubwa
kushinda wangu, huo ndio
ushindani wa kweli, hata hivyo
siwezi kuwa juu milele.”
0 comments:
Post a Comment