MKALI wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Mbwana
Mohammed maarufu kama
Mb Dogg, yupo kwenye
mipango ya kuachia wimbo
wake mpya unaokwenda kwa
jina la Baby mbona
umenuna?
Mb Dogg pichani, wimbo
wake mpya wa 'Baby Mbona
Umenuna' utakuwa balaa na
unatarajiwa kumuweka tena
kileleni.
Wimbo huo umerekodiwa
katika Studio za Maccopa,
ambapo unatarajiwa
kurudisha makali na heshima
ya msanii huyo aliyewahi
kuwika katika tasnia hiyo.
Akizungumza jana jijini Dar
es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Qs Mhonda J
Entertainment, Joseph
Mhonda, alisema kwamba
wimbo huo ni moto wa
kuotea mbali ambao kwa
kiasi kikubwa utamuweka
juu zaidi.
Alisema kwamba Mb Dogg ni
msanii aliyejichimbia kwa
muda mrefu akiwa na
mahitaji ya kurudi kwenye
nafasi zake za juu alipokuwa
awali.
“Sisi kama Kampuni
tunaofanya kazi na Mb Dogg
tunaamini kabisa huu ni
wakati wake wa kurudi tena
kileleni ili aendeleze makali
yake ya awali.
“Baby Mbona umenuna ni
wimbo ambao kwa hakika
utadhihirisha ubora wa
mwimbaji huyu wa Latifa na
nyinginezo zilizomuweka
kileleni,” alisema.
Mb Dogg anatokea katika
kampuni hiyo kwa sasa,
akiwa sambamba na Nay wa
Mitego anayetamba na
wimbo wa Muziki Gani,
aliyeimba na Diamond.
0 comments:
Post a Comment