STAA wa nyimbo za Injili Bongo,
Rose Muhando yamemkuta ya
kumkuta ambapo Ijumaa iliyopita
alishikiliwa na Polisi wa Kituo cha
Msimbazi jijini Dar es Salaam
kwa madai ya kuingia mitini na
shilingi milioni 6 alizolipwa kwa
ajili ya kwenda kufanya shoo ya
kiroho, Mombasa, Kenya
Novemba 3, 2013 lakini
hakutokea. Kwa mujibu wa
chanzo chetu, Rose alidakwa jijini
Dar es Salaam saa sita mchana
huku mlalamikaji wake akiwa ni
mtu aliyejulikana kwa jina la
Nathan Wami.
Nathan amewahi kuwa meneja
wa kazi za Rose Muhando. Kwa
sasa Rose anaratibiwa na
Kampuni ya Sony.
MADAI YA JALADA LA KESI
Kwa mujibu wa chanzo, jalada la
kesi hiyo lilifunguliwa Dodoma
likisomeka; DOM/RB/1129/2014
KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA
UDANGANYIFU.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Rose
aliachiwa kwa dhamana akitakiwa
kurudi kituoni hapo Februari 8,
2014 huku mkononi akiwa
ameshika kiasi hicho cha fedha
kwa ajili ya kumlipa mlalamikaji
huyo.
WIKIENDA LATINGA POLISI
MSIMBAZI
Baada ya kuinyaka nyeti hiyo,
Ijumaa Wikienda lilipiga hodi
kituoni hapo na kuulizia kama ni
kweli nyota huyo wa wimbo wa
Utamu wa Yesu alishikiliwa.
“Sisi si wasemaji wakuu wa polisi,
hatuna mamlaka hayo. Hatuwezi
kusema ni kweli au si kweli,”
afande mmoja alilijibu gazeti hili.
MADAI NYUMA YA PAZIA
Wakati madai ya Rose yakiwa
hayo, nyuma ya pazia kuna
mlolongo wa matukio ya
kushangaza kati ya mwimbaji
huyo na Nathan.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja,
Rose amekuwa akiingia kwenye
madai ya kupokea fedha za shoo
na kutokwenda lakini Nathan
akielekezewa lawama zote.
PESA APOKEE MENEJA, LAWAMA
ABEBESHWE ROSE
“Jamani mimi nataka kuwaambia
ukweli, Rose hahusiki na hiyo
tabia. Wengi wanasema ana
mchezo wa kuchukua fedha za
watu halafu haendi kwenye tukio
lakini ukweli si huo,” kilisema
chanzo hicho.
Wikienda: “Ukweli ni upi? Funguka
basi.”
Chanzo: “Ukweli ni kwamba,
Nathan amekuwa akimnyanyasa
sana Rose kwa muda wote
aliokuwa meneja wake.
“Ilifika mahali, Nathan ndiye
alikuwa akipokea pesa kutoka
kwa watu wanaomhitaji Rose bila
kuwasiliana na mwenyewe.
Wakati mwingine Rose hajulishwi
mapema.
“Siku akiambiwa, pengine
anaumwa au yupo mbali na eneo
la tukio, sasa hapo waandaaji
wanamsema Rose kwamba
amechukua fedha na kuingia
mitini,” chanzo kilizidi kuweka
wazi.
ROSE HANA CHA KUFANYA
Kwa mujibu wa chanzo, hali hiyo
imekuwa ikimsumbua sana Rose
kwani ni kweli wengi wanaamini
hivyo lakini ukweli ni kwamba
anasingiziwa tu, Rose hawezi
kupokea fedha halafu asiende
kuimba ila kwa sababu Nathan ni
meneja wake aliyemtoa kisanii
anajikuta hana la kufanya.
“Mbona kwenye matamasha ya
Pasaka na Krismasi
yanayoandaliwa na Msama
Promotion hatujawahi kusikia
Rose kaingia mitini? Ni kwa
sababu Msama mwenyewe
anawasiliana naye moja kwa
moja,” kiliendelea chanzo.
NATHAN ALIISHI NA ROSE KWA
UBABE
Ikazidi kudaiwa na chanzo chetu
kwamba katika kipindi chote,
Nathan amekuwa akiishi na Rose
kwa ubabe wa hali ya juu, jambo
ambalo lilimuathiri Rose
kisaikolojia bila kujijua.
“Kuna mengi sana, tena yale ya
ndani zaidi, sipendi kuyasema
lakini Nathan mwenyewe
anayajua, siku ikifika nitayalipua
kama atapinga,” kilisema chanzo.
ROSE MUHANDO HUYU HAPA
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Rose
kwa lengo la kutaka kumsikia
atakachokisema juu ya madai
yote hayo kuhusu yeye na
Nathan, lakini zaidi ya yote tukio
la kuwekwa mahabusu ya
Msimbazi Polisi, msikie:
“Kusema ule ukweli mimi
namwachia Mungu, yeye anajua
ukweli uko wapi na uongo uko
wapi!”
NATHAN SASA
Baada ya hapo, gazeti hili
lilimtafuta Nathan Wami na
kumsomea mashitaka yote.
Nathan: “Hayo madai si ya kweli.
Kama kasema yeye siyo kweli.
Nimeishi na Rose karibu miaka
kumi na mbili, nilikuwa
namchukulia kama mtoto wangu.
“Nimekuwa nikiona kwenye
magazeti kwamba eti alisaidiwa
na mfuko wa kanisa wakati mimi
ndiye niliyemtoa.”
Wikienda: “Kwa hiyo madai
kwamba umekuwa ukiishi naye
kibabe, hukuwa unamtendea haki
si ya kweli?”
Nathan: “Si ya kweli hata kidogo.”
MSAMA ANAMLIPA NANI?
Gazeti hili liliwasiliana na
muandaaji wa matamasha ya
Pasaka na Krismasi, Alex Msama
kuhusu malipo ya Rose
Muhando.
Msama: “Mimi huwa namalizana
na Rose.”
Wikienda: “Kuna mwaka umewahi
kumlipa pesa halafu hakutokea
kwenye tamasha lako?”
Msama: “Hapana, hata Tamasha
la Pasaka mwaka huu atakuwepo
panapo uzima maana
tumeshamalizana.”
KUTOKA KAMPUNI YA SONY
Habari zilizopatikana kutoka
Kampuni ya Sony ambayo
inamratibu Rose kwa sasa,
zinasema kuwa wakati wa kuingia
makubaliano na nyota huyo
walikutana na masuala hayo ya
madeni lakini walipofanya
uchunguzi wakagundua mambo
ambayo hawakutaka kuyaweka
wazi lakini kimsingi
walimhurumia Rose.
“Ila mabosi wa Sony waliamua
kuwa yale madeni yaliyopita
watayalipa wao, yale ambayo
tarehe za Rose kuimba bado,
wamemwambia akaimbe ili
kumalizana na wahusika,”
kilisema chanzo hicho na kuomba
kutotajwa jina gazetini.
-GPL
0 comments:
Post a Comment