Wakati Keya Kazungu alipofanya
ziara ya kurudi katika mji wa
nyumbani kwenye Kaunti ya Kwale
kwa ajili ya mapumziko ya
Krisimasi, aliona mabadiliko ya
kipekee.
Mwezi Januari 2011 wakati
alipoondoka kwenda kusoma Chuo
kikuu cha Nairobi, alisema vijana
wa jirani kutoka dini mbalimbali
yalijichanganya pasipo shida,
wakizungumza wakati wa jioni.
Wakati aliporudi, Kazungu,
mwenye umri wa miaka 25,
alisema aligundua kwamba
marafiki zake walikusanyika kwa
mujibu wa mashirikisho ya dini
zao.
Pasipo kutambua mvutano wa
kidini ulioshamiri, Kazungu,
Mkristu, alisema aliungana na
kikundi cha rafiki zake Waislamu.
"Nilifurahi kuwaona kwani
hatukuwa tumeonana kwa kipindi
cha karibia miaka miwili," Kazungu
aliiambia Sabahi. "Nilitarajia
wangekuwa na furaha pia, hata
hivyo, rafiki zangu walikuwa
tofauti. Kwa dakika kadhaa kikundi
kilitawanyika kwenda eneo
lingine."
Hassan Mwalulu, mwenye umri wa
miaka 24, mkaazi Mwislamu wa
Kwale, alithibitisha kwamba
shughuli za kijamii ziliathiriwa na
mvutano wa kidini katika eneo
hilo.
"Vijana ambao walikuwa wakicheza
pamoja bila kujali dini zao kwa
sasa wanaenenda tofauti,"
aliiambia Sabahi.
"Vilabu vya ndani vya mpira wa
miguu vimeundwa kwenye
mwelekeo wa kidini," alisema,
akiongezea kwamba miezi
michache iliyopita mashindano ya
ndani ya michezo yalikuwa na
maovu ya mtindo wa kidini na wa
kimadhehebu.
"Ni jambo la kawaida kusikia timu
ikisema kwamba 'tutawaonyesha
hawa Wakristo namna mpira wa
miguu unavyochezwa' au
'tutawashinda hawa Waislamu,'"
alisema. "Michezo kama ya mpira
wa miguu inajulikana kwa
kuzidisha mambo mengi ikiwa ni
pamoja na dini, lakini siyo Kwale."
Kubadilisha mwelekeo huo, vikundi
visivyo rasmi na watu binafsi
wanahamasisha shughuli za
mwingiliano baina ya dini katika
kaunti hii, Mwalulu alisema.
"Waliandaa zoezi la kusafisha mji
mara mbili na mashindano ya
[mpira wa miguu] ambapo
wachezaji kutoka imani mbalimbali
wanachanganyika kuunda timu,"
alisema, akiongeza kwamba
jitihada zinaonyesha matunda
taratibu wakati mvutano
unapungua.
Zaidi ya hayo, alisema, vijana
wanakutana katika mikutano
mbalimbali ili kujadili masuala
yanayoiathiri kaunti na jinsi
yanavyoweza kushughulikiwa
vizuri.
"Tumeishi kwa pamoja kwa [muda]
mrefu ili kuruhusu baadhi ya
masuala kutugawanya," alisema.
"Nina marafiki Wakristo ambao
niliwaalika kupata pamoja chai na
vitafunwa nyumbani kwangu au
sehemu ya kulia chakula. na wao
walifanya hivyo hivyo. mvutano
huu wa dini ni suala la kupita.
Tunajitolea kurudisha undugu."
Mauaji ya wahubiri wa dini
yaharibu uhusiano
Hussein Khalid, mkurugenzi
mtendaji wa Haki Africa, asasi
isiyo ya kiserikali ambayo
inatangaza haki za kijamii na
kiuchumi kwa Wakenya wote,
aliiambia Sabahi kwamba mauaji
yasiyo na ufumbuzi ya wahubiri wa
Kiislamu na kikristo yalikuwa
yanaharibu uhusiano.
Khalid alisema serikali inaweza
kupunguza mvutano wa kidini kwa
kuchunguza na kuwashtaki
watuhumiwa wa mauaji ya
mapadri wawili wa Kikatoliki na
wahubiri saba wa Kiislamu katika
mkoa wa Pwani tangu 2012.
Ukosefu wa mashtaka umeongeza
mvutano katika dini mbili, ambazo
matokeo yake wafuasi wake
wamekuwa wakituhumiana wao
kwa wao, Khalid aliiambia Sabahi.
"Tunahisi kwamba vikosi vya ulinzi
vinahusika na mauaji ya watu
wanaotuhumiwa kuwa na
uhusiano na magaidi lakini
wanasababisha matatizo zaidi kwa
jamii ambazo zimekuwa zikiishi
pamoja kwa miaka mingi,"
alisema.
Kamishna wa kaunti ya Kwale
Evans Achoki alikanusha tuhuma
kwamba serikali ilikuwa inahusika
na mauaji nje ya mahakama ya
watuhumiwa wa ugaidi.
"Sote tumeshangazwa na mauaji
lakini uchunguzi unaendelea,"
aliiambia Sabahi. "Hatutoi nafasi
yoyote. Baadhi ya magaidi
wanaweza kuwa wanawalenga
wahubiri katika mpango wa
kuchochea mivutano ya kidini."
Mwenyekiti wa Baraza la Wahubiri
wa Dini mbalimbali wa Pwani
Padri Wilybard Lagho alikiri
kulikuwa na kuongezeka kutengana
na kutovumiliana baina ya imani
tofauti.
Uhusiano kati ya Waislamu na
Wakristo katika mkoa wa Pwani
umetetereka, aliiambia Sabahi.
Msingi wa kuondoa kutokuwa na
uvumilivu wa kidini ni kuendelea
kuonyesha umoja miongoni mwa
viongozi wa dini, alisema,
akiongeza kwamba watumishi
kutoka imani zote wanafanya kila
wawezalo kuboresha uhusiano.
Licha ya kufanya kazi tofauti na
jamii zao, ushirikiano kati ya
Waislamu na Wakristo unahusisha
kuonekana pamoja katika
mikutano inayofanyika katika
ukumbi wa mji na barabarani
kuhubiri amani na umoja , alisema
Lagho.
"Hatuelewi kiwango cha kutokuwa
na uvumilivu, lakini pamoja na
maulamaa wa Kiislamu
tunaonekana kwa utulivu na
uvumilivu pamoja na imani zetu
zinazohusika. Tunaamini kwamba
kutokuwa na uvumilivu wa dini
hakutapunguza vurugu za kisekta,"
alisema Lagho.
Lagho alisema Wakristo
wanahamasishwa kujichanganya
na kufanya biashara pamoja na
Waislamu.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Ushauri la Waislamu Kenya Sheikh
Juma Ngao alisema Maulamaa wa
Kiislamu wataendelea kutetea njia
zisizosababisha vurugu kwa
kutatua mambo.
"Dini zote zinamhitaji kila mmoja
kwa ajili ya ustawi wa dini na nchi
kwa ujumla," aliiambia Sabahi.
"Kuna njia ambazo zinahitaji
kutumika … Bila kujali mtu alikosa
kiasi gani, sio haki kufanya hivyo
kwa mtu wa imani tofauti."
Ngao alisema maimamu kutoka
katika misikiti mbalimbali
wamekubali kusisitiza mada hiyo
ya umoja na uvumilivu wakati wa
mahubiri yao.
"Kuwepo kwa amani ndiyo
kulikuifikisha nchi umbali huu na
tunawajibika kuudumisha,"
alisema.
0 comments:
Post a Comment