ads

Tuesday, February 18, 2014

P FUNK MAJANI

11:43 AM By Unknown

P Funk Majani amewapa makavu
watu wanaochonga kuhusu
maendeleo yake hususani wale
wote ambao wanapiga majungu
kuwa mkali huyo amepotezwa na
vijana wadogo kwenye industry
ya mziki.
“Kuna watoto wadogo siku hizi
wanakurupuka wanajiona wao
ndio wao, juzi kati nikiwa kwenye
club moja nasikia kiproducer
kinachonga kuhusu mimi
kenyewe kana sijui nyimbo moja
au tatu zimehit mimi nina
nyimbo zaidi ya 100 ambazo
zimehit na hadi akina Mhe Mkapa
enzi hizo, wametukubali we
utaniambia nini” P funk alinena.
Majani amefunguka kuwa kuna
watu wanamtafuta chuki ili
kumpachika skendo akitolea
mfano msanii wa kizazi kipya Ney
wa Mitego kuwa haelewi kitendo
cha rapper huyo kumtukana
kwenye nyimbo yake kulikua na
lengo gani kwasababu msanii
huyo hamkaribii hata kidogo kwa
level zake.

0 comments:

Post a Comment