ads

Sunday, February 16, 2014

JK AWATAKA WANACHAMA WAKE WAVUNJE UKINMYA ZIDI YA KUONEWA KWAO NA WANACHAMA PINZANI

6:43 AM By Unknown , No comments

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya
Kikwete amewataka wanachama
wake kuacha unyonge na kujibu
mapigo ya wapinzani hasa wale
ambao wanaendesha siasa za
vurugu katika kampeni za chaguzi
mbalimbali nchini.
Rais Kikwete amesema kuwa
uvumilivu una ukomo, na kwamba
sasa wanachama wa CCM hawana
budi kuacha unyonge, kutokana na
siasa hizo za vurugu
zinazoendeshwa na vyama vya
upinzani.
Aliyasema hayo jana mjini hapa
wakati akifungua kikao cha
kawaida cha Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya CCM
kitakachokutana kwa siku mbili
chini ya uenyekiti wake, ambacho
ajenda kuu ni kuzungumzia Bunge
Maalumu la Katiba.
“Tumelizungumzia hili katika
Kamati Kuu, tumekubaliana kuacha
unyonge (makofi). Ndio watu
wamelisema hili katika Kamati
Kuu, tumesema jamani
tumekubaliana kuacha unyonge,”
alisema Rais Kikwete ambaye
wakati anafungua kikao hicho
waandishi wa habari walikuwamo,
na akaongeza: “Wacha wakaseme
(waandishi wa habari), ndio
tumekubaliana kuacha unyonge.
Kabisa. Hata kama leo katika
taarifa za habari, zisiwekwe habari
nyingine, msikike ninyi tu.
Uvumilivu una ukomo wake.”
Mwenyekiti huyo wa CCM alisema
wamefikia hatua hiyo kwa sababu
yanayotokea yanasikitisha sana na
akatoa mfano wa matukio kadhaa
ya uvunjifu wa amani katika
kampeni katika maeneo ya Igunga
mkoani Tabora na Kahama mkoani
Shinyanga.
“Maana tunashindana na wenzetu
wagomvi maana wao ugomvi ndio
sehemu ya mwongozo wa kufanya
kazi ya siasa. Maana pale Kahama
kijana wamemtoa macho kwa
bisibisi. Acheni unyonge (makofi).
“Nasema kwa kweli kwa sababu
yanayotokea yanasikitisha. Pale
Igunga kijana yule wamemmwagia
tindikali, pale Kahama kijana
wamemtoa macho kwa bisibisi.
Tuache unyonge,” alisisitiza Rais
Kikwete huku akishinikizwa kwa
shangwe za CCM Oyee, Mapinduzi
Daima.
Ingawa Rais Kikwete hakutaja
chama, Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimekuwa
kikihusishwa na vurugu za
uchaguzi katika maeneo
mbalimbali yakiwamo ya Igunga
na Kahama katika uchaguzi mdogo
wa madiwani uliofanyika hivi
karibuni na pia katika chaguzi
ndogo za ubunge.

0 comments:

Post a Comment