ads

Saturday, February 22, 2014

UTANDAWAZI UMEKUWA NI CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI YA WANAFUNZI BARANI AFRIKA

9:38 AM By Unknown , No comments

HABARI za tokea wiki iliyopita. Ni
matumaini yangu kwamba
wanafunzi mnaendelea vizuri na
masomo na wasomaji wengine
wa safu hii Mwenyezi Mungu
anawabariki ili mambo yetu
yaende sawa sawa.Hili ni kama
hitimisho la mada yetu, ile
tuliyojadili kuhusu chanzo hasa
cha watu wazima kujihusisha
kimapenzi na watoto wa shule,
hasa wa sekondari na vyuo.
Kama ilivyotokea wiki iliyopita,
idadi ya wadau waliowasiliana na
mimi ilikuwa kubwa na uchangiaji
wao wa mada ulikuwa ni wa
kupendeza kabisa.
Kama ilivyokuwa awali, bado
lawama zilielekezwa kwa pande
zote mbili, yaani wapo
waliowalaumu vijana wa shule na
wale watu wazima. Mtakumbuka
tulijaribu kuuliza ni kitu gani
kifanyike, ambacho kwa maoni
yenu kinaweza kupunguza tabia
hii, kama siyo kumaliza kabisa.
Ingawa kila mmoja alijitahidi
kushauri vile anavyoweza, lakini
kwa ujumla watu wote walielekea
kuamini kuwa endapo tamaa
ikiepukwa, ya kihali na kimwili,
kati ya wanafunzi na watu
wazima, tatizo hili linaweza
kupungua kwa kiwango kikubwa.
Watoto wa kike wakiondoa tamaa
za maisha mazuri na kupata vitu
vinavyowazidi umri, kama vile
simu za bei mbaya na wazazi nao
wakiamua kudhibiti tamaaa zao
za mwili, upo uwezekano wa
kuondoa tatizo hili.
Utandawazi nao umechangia
sana watu kubadili aina ya
maisha tunayoishi. Tofauti na
zamani, ambapo mtoto mdogo
alikuwa ni mali ya jamii husika,
sasa hivi jukumu la kulea na aina
ya maisha limeachwa kwa mzazi.
Ndiyo maana wakati wapo baadhi
ya watoto wanamiliki simu za bei
mbaya walizonunuliwa na wazazi
wao, wapo wanafunzi ambao
hawatakiwi, siyo tu kumiliki, bali
kukutwa na chombo hicho cha
mawasiliano wakiwa bado shule.
Hata wazazi nao, hawaonekani
kuvutiwa na ule msemo wa
mtoto wa mwenzio ni wako pia,
wanawakuza wa wenzao na
kujisikia fahari kutembea nao.
Mtu mmoja alipendekeza watu
kumrejea Mungu, kwani mambo
haya ya ukisasa, yametufanya
sasa tusione haya kuwa na
wapenzi ambao tumepishana
sana.
Zifuatazo ni baadhi ya sms za
wasomaji wengine na
mapendekezo yao.
“Mimi ni dereva wa chuo kimoja
cha Biblia, karibu yetu kuna
shule moja ya sekondari, siku
moja nilipokuwa natoka tu na
gari niliwaona wanafunzi wawili
wanaokaa nilikokuwa naelekea,
nikasimama na kuwapa msaada,
mmoja akaomba simu ampigie
ndugu yake baada ya kuiona
ndani ya gari, nikampa si
akajibip, nikamuuliza mbona
anajibip akasema mawazo sijui
yalikuwa wapi, baada ya hapo
alianza kunitumia sms
mbalimbali, nilipogundua shida
yake nikamtaka tukutane, unajua
nilimpeleka kanisani na
nikamwambia hapa ndio
nyumbani kwetu, nikamtaka
aokoke, nikamfanyia maombi, je
kama ningekuwa sijaokoka!
Miye kwa maoni yangu tufanye
hivi, ili tuweze kukomesha yule
mtu anapokuwa gesti, yaani
mapokezi inatakiwa awe
anatazama umri wa mzee na
denti mwenyewe, je huyu denti
anaweza kweli kushea love na
huyo mzee? Kama ataona
haiendani hiyo love basi
amwambie yule baba au denti
mwenyewe kuwa hampaswi
kuingia kwenye chumba, akikataa
huenda hiyo itasaidia.
Kama nilivyochangia kuwa hili
jambo ni Comprehensive sana,
udhibiti wake unahitaji nguvu
kubwa mno kwani uhuru mkubwa
tulionao ambao umechangiwa na
Globalization pamoja na social
influence inakuwa si rahisi sana,
ila tunapaswa tu kumrudia
Mungu na kurejea maadili yetu ya
kiasili. Nyorido H A, Kisongo
Arusha.
Anko miye naona wazazi wawe
makini na watoto wao, pia
wanafunzi wajitambue, waache
kujidhalilisha kwa watu wazima.
Mwanafunzi unawezaje
kuchanganya elimu na masomo?
Jamani wanafunzi amkeni kuweni
makini, magonjwa ni mengi sana
na pia wanafunzi anaweza
kuharibu maisha yake endapo
atapata mimba na hao watu
wazima huwa hawakubali hizo
mimba.
Anko hili tatizo kiukweli siyo
rahisi kama unavyodhani,
kilichopo sisi wenyewe tuingiwe
na ubinadamu kuwa mtoto wa
mwenzio ni mwanao na baba wa
mwenzio ni baba yako na siyo
baba mkubwa wala mdogo, ni
baba yako mzazi, hapo
tutakapoonesha kizazi hiki na
kijacho. Tofauti na hapo anko
tuking’ang’ania baby, baby,
tutakuja kukosa ushahidi kweli.

0 comments:

Post a Comment