Inakadiriwa takriban watu milioni
moja na nusu wanaishi na virusi
vya HIV na maradhi ya UKIMWI
nchini Kenya.
Wavuvi vijijini huwapa wauza
samaki wanawake samaki kama
malipo kwa kufanya nao ngono
badala ya pesa.
Lakini sasa mashirika ya misaada
yanajaribu kubadilisha tabia hii,
ijulikanayo kama 'kubadilisha
ngono na samaki'.
Wanawahimiza wanawake
wanunue mashua zao wenyewe.
Mariam Omar ana zaidi toka
magharibi mwa Kenya.
0 comments:
Post a Comment