ads

Monday, February 24, 2014

MWANA DADA MREMBO AFIA GEST JIJINI ARUSHA

11:29 PM By Unknown , No comments

MREMBO mmoja ambaye alihu-
dumu kwenye nyumba ya kulala
wageni na baa (jina tunalo)
iliyopo Tengeru, wilayani
Arumeru, mkoani Arusha,
Blandina Michael (33) amekutwa
amekufa kwenye moja ya vyumba
vya nyumba hiyo huku chanzo
cha tukio hilo kikihusishwa na
vitendo vya ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu
mmiliki wa nyumba ya wageni
moja ambaye pia anajihusisha na
biashara za madini (jina tunalo)
kwamba alimtoa kafara
mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa,
kila mwaka mtu mmoja katika
biashara zake hupoteza maisha
ghafla.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo
alipoongea na Uwazi juzikati
alikanusha vikali tuhuma hizo na
kueleza kuwa yeye ni muumini
mzuri wa imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana,
unajua kuna mwaka mwanaume
mmoja alikufa ghafla kwenye
nyumba yangu ya kulala wageni,
alikuja na mpenzi wake ila
alimeza Viagra ambazo hata
polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na
mimi tukio hilo wanaliunganisha
na hili kwamba nawatoa kafara,”
alisema.
Kifo cha Blandina kilitokea ndani
ya chumba huku mtu mmoja
anayedaiwa kuwa mpenzi wake
aliyejulikana kwa jina moja la
Timo, mkazi wa eneo hilo
akihojiwa na polisi.
Marehemu Blandina ambaye ni
mzaliwa wa mkoa wa Tanga,
anaelezwa na bosi wake huyo
kwamba alikuwa kama mtoto wa
familia yake kwa vile alimwamini
sana. Alifanya kazi hapo kwa
miaka 8 na hakuwa na tatilo la
kiafya.
Bosi huyo alisema mwili wa
marehemu uligundulika baada ya
mfanyakazi mwenzake wa kiume
kumpigia simu saa 2 asubuhi
ambapo simu yake ilikuwa ikiita
bila kupokelewa ndipo alipoamua
kwenda kumgongea katika
chumba hicho.
Alisema baada ya kufika
alishangaa kukuta mlango wa
chumba chake uko wazi na
alipochungulia alibaini kwamba
Blandina alikuwa amefariki dunia.
Hata hivyo, polisi baada ya kufika
na kuufanyia uchunguzi wa awali
mwili huo hawakugundua
kuwepo kwa jeraha lolote
linaloashiria kuuawa, ingawa
mwili huo ulipelekwa kufanyiwa
uchunguzi wa kitaalam katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru.

0 comments:

Post a Comment