ads

Saturday, March 1, 2014

Whatsapp YAJA NA KASHESHE HIVI KARIBUNI LA KUWAUMBUA WAONGO

12:25 AM By Unknown , No comments

Kasheshe tena bonge la
kasheshe laja. Kwa kutumia
maspy wake wa kimataifa,
blog yenu mzigo imekuja na
taarifa ambayo italeta
usumbufu mkubwa katika
jamii ya watumia whatsapp
hapa Bongoland. Najua
mnajiuliza ni nini? Hata sisi
wakurugenzi, waandishi,
wafagizi wa hii blog ya
chekanakitime tuliduwaa
hivihivi kama wewe
ulivyoduwaa wakati tunasubiri
kuelezwa na spy wetu wa
kimataifa ni nini alichogundua
kuhusu watumiaji wa
Whatsapp.
Baada ya Whatsapp kuwa na
kale kamtindo kabaya ka
kuumbua watu kakusema 'Last
seen 2:00'na hivyo kuua kale
kakisingizio kuwa simu ilikuwa
imezima kwa kukosa chaji sasa
wanakuja na mpya zaidi. Kale
kakipengele katakuwa
kanataja hata ulipo, hivyo
katakuwa kakisomeka
mfano,'Last seen 2:00 Sokoni
Kariakoo'.
Sasa hii ni mbaya sana wakati
mtu kakutumia mesej...Baby
tumekusanyika hospitali
mamake rafiki yangu yu
mahututi' Huku Whatsapp
inakuonyesha 'Last seen 2:00
Coco Beach'... Kamtindo haka
kanategemea kuua mapenzi na
ndoa kadhaa ambazo mpaka
sasa zinaonekana kuwa imara
sana.

0 comments:

Post a Comment