ads

Monday, February 24, 2014

COVER YA FILAMU YA MPONZA DR.CHENI

9:20 PM By Unknown , No comments

Msanii wa filamu hapa nchini
anayefahamika kwa jina la Dr.
amejikuta katika wakati mgumu
baada ya bodi ya filamu Tanzania
kuzuia filamu yake mpya inayoitwa
'Nimekubali Kuolewa' kwa madai
ya cover iliyotumika katika kasha
la filamu hiyo inachochea ushoga.
Kufuatia madai hayo msanii huyo
amesema kuwa
bodi hiyo haikumtendea haki kwa
kuwa filamu yake ina lengo zuri la
kupinga ushoga na sio kuchochea.
Ameela bodi hiyo haikuangalia
maudhui na badala yake
imeangalia zaidi cover la filamu
hiyo
“Eti ushoga wangu uko kwenye
kujiremba sana, wamenionea,
lengo letu ni kukemea na kupinga
vikali vitendo vya ushoga na ndoa
za jinsia moja, huwezi kuelimisha
bila kuonesha madhara yake kwa
vitendo kama ilivyo kwenye filamu
hiyo. Amesema Dk Cheni.
Msanii huyu amekumbwa na hali
hiyo ikiwa ni muendelezo wa bodi
ya filamu kuzuia filamu ambazo
inazitilia mashaka.
Hata hivyo bodi hii imekuwa
ikilalamikiwa na baadhi ya wasanii
wakidai haitendi haki.

0 comments:

Post a Comment