Shirika la Misaada kwa watoto,
Save the Children, linasema
kuwa watoto milioni moja
hufariki dunia kila mwaka
katika siku yao ya kwanza ya
maisha.
Katika ripoti mpya ya shirika hilo
la misaada kwa watoto linasema
vifo vya watoto wachanga
vimesalia kuwa moja ya aibu za
dunia ya sasa.
Hali ya watoto ni mbaya zaidi
hasa katika mataifa
yanayokabiliwa na mizozo.
Mwandishi wa BBC aliye Sudan
Kusini, Anne Soy, amesema kuwa
katika mazingira ya sasa ya Sudan
Kusini, watoto na wanawake, hasa
wale waja
wazito wanaokabiliwa na athari
nyingi za vita vinavyoendelea
nchini humo.
Amesema kuwa kutokana na vita
watoto, walioandamana na wazazi
wengine wakiwa pekee,
wanaungana na akina mama
kutembelea mwendo
mrefu ili kujiepusha na vita vya
kikabila vinavyoendelea nchini.
Miundo msingi katika Sudan
Kusini, kama vile hospitali ni
chache sana jambo ambalo
linatatiza maisha ya wanawake na
watoto.
Katika hospitali ya mji wa Nimule
kwenye mpaka wa Sudan Kusini
na Uganda Kuna vitanda 174
pekee hospitalini idadi ambayo
haiafikiana kamwe
na maelfu ya wagonjwa na
wahasiriwa wa vita .
Save the children inasema kuwa
vita vinawaathiri zaidi watoto
huko Syria, Jamhuri ya Afrika ya
Kati CAR na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Shirika la Save the Children
linasema kuwa vifo hivi vingi
vinaweza kuzuiliwa.
0 comments:
Post a Comment