WATU wawili wa familia moja
wameuawa wilayani Maswa
mkoani Simiyu, kwa kupigwa na
wananchi waliojichukulia sheria
mikononi, wakiwatuhumu kuzuia
mvua kunyesha hivyo kusababisha
ukame kwenye eneo lao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Simiyu, Charles Mkumbo alitaja
waliouawa ni Gilya Chile (70) na
mjukuu wake, Nyangu Nyambalya
(30).
Polisi inashikilia watu wanane
akiwemo Kamanda wa
Sungusungu, Sosoma Masamuda
(50), Ligwa Malimi wakituhumiwa
kuhusika na mauaji hayo.
Wengine ni Emanuel Kasmiri (42),
Michael Sospeter (18), Toto
Emanuel (28), Nyanzobe Ntinga
(26) Tabu Zengo (31) na Joyce Kija
(30). Baada ya uchunguzi wa polisi
kukamilika, watafikishwa
mahakamani kujibu mashitaka.
Mauaji hayo yalifanyika usiku wa
kuamkia juzi katika kijiji hicho,
Kata ya Mwanhonoli wilayani
Maswa.
Inadaiwa sungusungu wa kijiji
hicho waliitana usiku na kuafikia
katika kikao chao kwenda
kuwaamsha babu na mjukuu wake
waeleze sababu za kuzuia mvua
kunyesha.
"Usiku huo walinzi hao wa jadi
waliwakamata watuhumiwa hao
waliokuwa wamelala nyumba
tofauti wakawahoji kwa nyakati na
maeneo tofauti na kuwataka
watoe maelezo ya kutosha ya
sababu ya wao kuzuia mvua
isinyeshe mpaka mazao kuanza
kukauka katika mashamba ya
wakulima wa kijiji hicho,’’ alisema
kamanda.
Inadaiwa sungusungu
hawakuridhishwa na maelezo
ndipo walianza kuwasulubu kwa
kipigo na kuwasababishia mauti
kabla ya kuteketeza miili yao.
Kamanda alisema, uchunguzi wa
awali wa polisi umebaini kabla ya
vifo vyao, watuhumiwa walikuwa
wakitamba kwenye vilabu vya
pombe kuwa wanatoka kwenye
familia ya kitemi hivyo wana
uwezo wa kuleta mvua au kuizuia
isinyeshe.
Kwa mujibu wa kamanda, tambo
hizo zilifanyika kipindi ambacho
kijiji hicho kilikumbwa na ukame.
Inadaiwa watu hao walishauri
wananchi wa kijiji hicho
wawachangie gunia moja la
mahindi au mtama kila kaya
walete mvua.
0 comments:
Post a Comment