MMMH mshaanza eti nimeisha
ingia mama Chaunabe kitanga na
njia nisiye na bleki kwenye domo
langu, wahenga wanasema
kinywa cha mkubwa kinanuka
lakini maneno hayanuki. Najua
maneno yangu ya shombo
huenda hayakufurahishi wewe
ambaye kila kukicha unabadili
wanaume na kuonekana una hila.
Shutuuu dada mwanamke tabia
babu wee, mwanamke kujua
mumeo anataka nini, mwanamke
kujituma kwenye kiwanja kifupi
cha sita kwa sita.
Unasahau cha kumvutia
mwanaume unakimbilia
kuukoboa mwili nani kakuambia
weupe mali? Basi mkaa usinge
nununuliwa!
Tena leo nakazi na wewe, nani
kakuambia weusi ni laana. Basi
leo nataka nikuambie wewe usiye
na haya uliyemaliza vipodozi
mwisho wa siku uso
unakuparama kama mchawi
mzee, unalo hilo?
Siri ya weusi maana yake ni
utamu hata zambarau tamu ni
nyeusi, zabibu tamu ni nyeusi na
hata usingizi mtamu unapatikana
usiku mweusi. Huoni Mzungu
akimuonja mswahili
anachanganyikiwa.
Wewe unajikoboa Mzungu ajipake
masizi? Acha ubwege. Nimejikuta
hata nikisahau kuelezea
nilichokikusudia kwa ajili ya
malimbukeni wachache, jivunie
weusi wako babu wewe.
Tuachane na hayo ambayo kwa
kiasi nimejikuta nikipandwa na
mzuka na kuingia kwenye mada
nyingine. Kama unabisha
mwangalie jirani yako
anayetumia mkorogo ngozi kama
kuku wa mayai aliyezeeka badala
ya kupendeza anabakia kituko
mtaani.
Acha niendelee na kilicho nitoa
nyumbani, shoga leo nilitaka
kukuelezea kitu kimoja
kuhusinana na tabia za baadhi ya
wanawake kukosa lugha tamu
ndani ya nyumba zao kushindwa
kuwalisha waume zao nyama ya
ulimi. Mwanamke unakosa lugha
tamu kwa mumeo hujui kusema
asante, hujui kusema samahani,
hujui hata kumsifia mumeo!
Mumeo akikuletea kitu
unakipokea na kuamnini ni
wajibu wake kukuletea una hiyari
ya kusema asante au kukaa
kimya. Lakini nataka nikuambie
shoga kitu kinacho mtuliza
mwanaume ni pamoja na
maneno matamu. Mfano amerudi
toka kazini baada ya kumpokea
lazima umpe pole ya kazi.
“Karibu mpenzi pole na kazi,”
akikujibu asante, mwambie.
“Yaani kila muda jicho langu
lilikuwa likitazama barabarani
utarudi saa ngapi mpenzi
wangu,” hata kama ulikuwa ndani
ukiendelea na kazi zako.
Vitu hivi humfanya mwanaume
kuamini kabisa hata anapokuwa
mbali nawe bado ulimuweka
moyoni mwako, siyo anakuja
baada ya kumpokea unabakia
kama bubu haipendezi, tumia
ulimi wako kumliwaza mumeo.
Mpo katika safari ya huba mkifika
pwani lazima mpeane pole na
asante kwa kusafiri salama,
pengine wewe umewahi mwenzio
naye anakufuata pwani msaidie
naye afike pwani na baada ya
kufika mpe pole pia kumpa
asante kwa kukusafirisha vyema
katika bahari ya huba.
Usiwe uvivu wa kuomba
msamaha unapokosa, hata kosa
lenyewe liwe dogo, kumbuka
kosa ni kosa na chanzo cha moto
ni cheche. Wapo wachache lugha
tamu huzitumia kwa muuza
genge ili apunguziwe lakini kwa
mumewe vitu hivyo havionekani.
Tumia ulimi wako kujenga
nyumba yako kumfanya mumeo
aone tofauti ya mwanamke wa
nje na mkewe ambaye kila neno
tamu na zuri humwambia
mumewe. Nyama ya ulimi
ukiitumia vizuri itakufanya kila
siku penzi lako lizidi kuwa tamu,
si wajinga waliosema sauti tamu
ilimtoa nyoka pangoni na
kumtuliza simba mwenye njaa.
Yangu si mengi kwa leo, ila
kumbuka wimbo mzuri
humbembeleza mtoto akalala.
0 comments:
Post a Comment