ads

Wednesday, February 5, 2014

JANGA JINGINE LAZUKA SHILOLE SIKIO LA KUFA, AKANA MAAGIZO ALIYOPEWA NA MCHUNGAJI

3:49 PM By Unknown , No comments

STAA wa mduara Bongo, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’ amedhihirisha
kuwa ni sikio la kufa baada ya
kusema yeye ni miongoni mwa
wanawake wanaojua kuchuna
mabuzi.
Kauli hiyo imechochea vigezo vya
kumfanya Shilole aonekane
hasikii kwani wiki kadhaa
zilizopita mchungaji wa kanisa
moja lililopo Ubungo, jijini Dar
ambaye hakujulikana jina lake,
alimtaka kuishi katika sura ya
kumpendeza Mungu lakini
inaonekana amempuuza.
Akizungumza na Risasi
Mchanganyiko juzi, jijini Dar es
Salaam, Shilole alisema alitunga
wimbo wa Nachuna Buzi kwa
sababu anajua kuwa wanawake
wengi ni mafundi wa tabia hiyo
akiwemo yeye mwenyewe!
“Unajua mwanamuziki unatakiwa
kuchagua wimbo ambao
unaigusa jamii nzima kwani
mambo ya kuchuna mabuzi kwa
wanawake yapo sana, hata mimi
mwenyewe ni mtaalamu wa
kuchuna mabuzi,” alisema
Shilole.
Hata hivyo alisema japokuwa ana
tabia hiyo lakini anatambua siyo
nzuri hivyo anawasihi wanawake
wengine kuachana nayo kwani
ipo siku itawaingiza matatizoni.
Mbali na mchungaji huyo, juzi
Jumapili, Mchungaji wa Kanisa la
Anglikana, Ukonga –Mazizini, Dar,
Emmanuel Kapande alimtumia
ujumbe wa watoto wa Shule ya
Jumapili (Sunday School)
nyumbani kwake kwa lengo la
kuimba na kufanya maombi.
Watoto hao walifika nyumbani
kwa Shilole, Mwananyamala -
Manjunju, wakiwa
wameongozana na walimu wao,
Jonas Timotheo, Rehema Ezra na
Catherine Libogoma.
Ujumbe huo, ulimpelekea baraka
ya maombi nyumbani kwake na
kumshauri aishi katika mazingira
yanayompendeza Mungu.
Katika hafla hiyo, vinywaji baridi
vilichukua nafasi yake huku
Shilole akipata nafasi ya
kuzungumza na watoto hao kisha
kupiga nao picha.

0 comments:

Post a Comment