AMA kweli dunia imefika
ukingoni! Ile Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) ya Global
Publishers, bado ipo kazini
ikishirikiana na polisi ambapo
safari hii imeibuka na kigongo
cha aina yake baada ya kumnasa
‘mwanaume tata’ akijihusisha na
ukahaba, Risasi Mchanganyiko
lina mzigo kamili.
Ikiwa kwenye fumuafumua ya
magenge ya ngono maeneo ya
Kahumba mjini Morogoro hivi
karibuni, OFM kwa mwaliko wa
jeshi la polisi, ilipigwa na butwaa
baada ya kukutana uso kwa uso
na mwanaume huyo aliyekuwa
amejumuika katikati ya kundi la
madadapoa naye akifanya kama
wao.
Mbali na jamaa huyo ambaye jina
lake halikupatikana, baadaye
ilibainika kuwa kulikuwa na
wenzake wawili ambao ilikuwa
vigumu kuwatambua kufuatia
kujiremba kupita hata wanawake
wenyewe.
Kuna madai kwamba kijana huyo
aliyekadiriwa kuwa na umri wa
kati ya miaka 20 - 24 ni mtoto wa
kigogo serikalini na amekuwa
akijichanganya na madadapoa
hao kwa muda mrefu.
Mara baada ya kunaswa, kijana
huyo aliangua kilio huku akidai
kuumbuka kwani familia yake
wakiiona picha yake
hawatamwelewa.
“Naombeni tumalizane hapahapa
kwani nyumbani hawafahamu
kuwa nipo hapa muda huu. Hii ni
kesi kubwa kwangu nisaidieni,”
alisikika kijana huyo.
Hata hivyo, pamoja na kilio
hicho, polisi hawakumwelewa,
alibebwa juujuu na kuingizwa
katika karandinga kisha kutupwa
nyuma ya nondo za mahabusu
kusubiri sheria kuchukua mkondo
wake.
Wakazi wa maeneo hayo
walikuwa wakilalamika mara kwa
mara kutokana na kurundikana
kwa makahaba mahali hapo na
kusababisha uchafuzi wa
mazingira kwa kutupa ovyo
mipira ya kiume (kondom).
Katika msako huo, wanaume hao
watatu walijumuishwa na
wanawake 20 waliokamatwa
wakijihusisha na biashara
haramu ya kuuza miili.
-GPL
0 comments:
Post a Comment