ads

Wednesday, February 5, 2014

UWANJA WA AZAM RUKSA KUTUMIKA KIMATAIFA KIMICHEZO

1:42 PM By Unknown No comments

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF)
limekubali Uwanja wa Azam uliopo
Chamazi kutumika kuchezea
michuano ya kimataifa. Kwa
mujibu wa taarifa iliyopo kwenye
mtandao wa Azam, CAF imekubali
uwanja huo kutumika kupitia
taarifa ya barua pepe iliyotumwa
juzi na Naibu Mkurugenzi wa
Mashindano Khaled Nassar.
Taarifa hiyo inasema, Uwanja wa
Azam umepita vigezo vyote
vinavyohitajika na CAF kuandaa
michuano ya kimataifa utaanza
kutumika katika mechi za Kombe
la Shirikisho ambayo Azam FC
wanashiriki.
Naye Ofisa Habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) Boniface
Wambura amethibitisha kuwa
Uwanja wa Azam umekubaliwa
kutumika katika michezo ya
kimataifa kwa klabu kuanzia
msimu huu.
"Ni kweli Uwanja wa Azam
umepata kibali cha kutumika
katika michezo ya kimataifa na
utaanza kutumika msimu huu
unakuwa uwanja wa kwanza
unaomilikiwa na klabu Afrika
Mashariki kuruhusiwa kuandaa
mashindano makubwa ya klabu,”
alisema Wambura.
Khaled ameandika katika taarifa
yake ya barua pepe kwenda TFF na
Azam FC kuwa CAF ilimtuma
mkaguzi wake toka Zimbabwe,
Wilfried Mukuna kuja kukagua
uwanja huo na Mukuna
aliwasilisha ripoti CAF iliyopelekea
shirikisho hilo kutoa kibali kwa
Azam FC na TFF kuruhusiwa
kuutumia uwanja huo kwa mechi
zinazoandaliwa na CAF.
Uongozi wa Azam FC umetoa
shukrani kwa mkaguzi wa CAF
Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya
Rais Jamal Malinzi na uongozi wa
CAF Cairo Misri hasa Nassar kwa
kuwezesha zoezi hilo kufanyika kwa
uwazi na uweledi wa hali ya juu.
"Pia Azam FC inapenda
kuwataarifu wapenzi wake kuwa
kuanzia msimu huu mechi zake za
CAF zitachezwa Azam Complex
Chamazi," ilisema taarifa ya Azam.

0 comments:

Post a Comment